Yuichi Ishii akiwa na miaka 38, ana watoto wengi kuliko mtu mwingine yeyote wa umri wake anayemfahamu.
Lakini hutumia takribani saa nne kwa siku kukaa nao, mara kadhaa wiki moja, inategemea na mahitaji ya wateja wake.
Miaka kumi iliyopita, Ishii alianzisha kampuni aliyoiita Family Romance, Kampuni inayokodisha 'familia na marafiki'.

Sasa kampuni ina waajiriwa 2,200 ambao hujifanya mababa na mama, binamu, wajomba, mabibi na babu na ndugu wengine bandia.
Umaarufu wa kampuni hiyo na uchangamfu wa mmiliki umekuwa ukikua tangu wakati ilipoanzishwa.
Leo hii Ishii ni ''baba''wa watoto 35 na anaiambia BBC anachojisikia kuwa sehemu ya familia 25 tofauti, bila kuwa na mahusiano nao ya kweli
Yuichi Ishii akiwa na suti nyeusi
'Bandia lakini kweli'
Ishii anasema sababu ya kuwa na wazo la kuanzisha kampuni ya Family Romance.Kwanza wazo lilikuja miaka 14 iliyopita wakati rafiki yake alipotaka kumpeleka mtoto wake wa kiume kwenye shule binafsi ya watoto ambayo ilitaka kuwahoji wazazi wote wa mtoto na mtoto mwenyewe.
Alikua mama pekee, hivyo Ishii akajiunga na mama huyo kwenda shuleni kwa mtoto.
''Njia hii haikufanikiwa kama tulivyotegemea kwa sababu mtoto na mimi hatukuweza kuigiza kuwa familia. Lakini nikafikiria kuwa kuna jambo zuri kuhusu suala la uhitaji wa familia.''
Family Romance, anasema, ''inatimiza mahitaji fulani ya watu wanaohitaji usaidizi.''
''Mimi ni mwanafamilia bandia, lakini kwa saa chache nitakuwa rafiki wa kweli au ndugu.''
Yuichi Ishii akwia na rafiki yake

Marafiki na familia wanakodishwa

Wateja wa Ishii wana mahitaji mbalimbali.
Watu wengine wanataka wapenzi wao wakutane na wazazi wao, na kwa sababu yeyote ile, hawawezi kuwatambulisha kwa familia zao za ukweli.
Katika mazingira hayo Kampuni hujaribu kuwapata watu wanaofanana na urefu wa mteja, rangi ya nywele na mwenye umri unaofaa.
''Watu walio na ugumu kuanzisha urafiki wanaweza kupata rafiki wa kukodi.'' anasema.
''Tunajifanya kama marafiki wa kweli, tunakwenda kufanya manunuzi pamoja, matembezini, na kupiga gumzo pamoja.''
Kuna watu wanakodi mabinti feki, watoto wa kiume feki, wajukuu, ili kufidia nafasi ya watoto waliowahi kuwa nao au kutokuwa nao kabisa.
Wengine hukodisha kwa ajili tu ya kuhudhuria sherehe.
Wazazi wakimtazama mtoto akitembeaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Baba ni nafasi muhimu

Lakini Ishii anasema nafasi ya Baba huwa inahitajika sana.
kuna takribani wanandoa 200,000 huachana kila mwaka nchini Japan na familia nyingi huishia kuongozwa na mzazi mmoja.
Ishii anasema, kama ilivyo kwa jamii nyingine, familia zinazoongozwa na mzazi mmoja zinakuwa na uhitaji, hivyo huduma ya kampuni yake husaidia ''kutimiza'' mahitaji ya jamii.
Lakini anaongeza, ''Hakuna aina moja ya hitaji linalohitajika na kila familia.''
''Baadhi ya wateja wanataka baba mpole, wengine mkali wengine mtanashati. Mzazi mkali, anaweza kuzungumza lahaja ya Kansai (inayosikika na ukali kuliko kijapani cha kawaida).''
Kama watoto ni wadogo, hadithi ya kudanganya itahitajika kueleza kuwa nini baba hakuwepo kipindi chote hicho.
Ugumu wa kazi ya Ishii ni kuja na sababu ya kuwaambia kwaheri watoto ambao aliojifanya baba yao.
''Si rahisi kuwashawishi watoto. Ni huzuni sana kumuona mtoto akilia. Hapa ni pagumu.
Mwanamke akitembea mtaaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Wafanyakazi wa Family Romance wanaweza kuwa na famili tano, lakini tangu Ishii alipoanzisha kampuni yake, kwa sasa ana familia 25.
Idadi ya watoto 35 ambao wanamuona kama baba yao wa kweli na ana mahusiano 69 ya uongo ya urafiki au udugu.
''Ninatakiwa kuhakikisha kuwa ninatazama maelezo ya kila familia kila siku kabla ya sijafika nyumbani kwao. Nina kitabu cha kuandika maelezo kikiwa na majina ya kila mmoja na taarifa zake ninazozitaka,''anasema Ishii.
''Wakati mwingine ninasahau majina yao ya utani au kitu kingine, hivyo huwa ninakwenda maliwatoni kutazama kitabu cha maelezo.''
Lakini hilo huwa halifanyi kushindwa kubeba majukumu ya mzazi, kama vile kuwapeleka watoto shule asubuhi, mikutano, matukio ya michezo jioni na chakula cha jioni.
''Ni kazi nyingi na sina mapumziko,'' anasema.
''Niliamua kuwa muda wangu binafsi ni kati ya usiku wa saa sita mpaka saa tisa, bila kujali nimechoka kiasi gani. Ninachora picha...hayo ndio mapumziko yangu. Ninalala takribani saa tatu kwa siku.''
Mwanamke na mwanaume wakiwa wameshikana mikonoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Biashara na hisia

Ishii hajaoa na hana watoto wa kuzaa- wala hataki kupata watoto.
Anafikiri kuwa, ikiwa ataanzisha familia yake, hataweza kumudu familia yake ya kweli na zile za kutengeneza 25.
''Watajisikiaje kama nitafunga ndoa?'' Ishii anasema
''Kama ningekuwa na watoto wa kweli, ningekuwa na hofu kuwaona kama familia bandia na kunivuruga.''
Ishii anasema, biashara yake inakuwa na makubaliano kati ya kampuni na mteja kuwa na mipaka kwenye mahusiano.
Hawawezi kupigana mabusu au kufanya tendo la ndoa, kwa mfano watashikana mikono tu. Kampuni inatoa huduma aina 30 na kila moja ina masharti yake.
Wateja hulipa kiasi cha dola 180 kwa saa nne za kampuni, usafiri na chakula. ''Si rahisi kwa mama ambaye ni kiongozi wa familia,'' Ishii anasema.
Mwanamke akitembea mtaaniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Ukweli unauma

Ishii anakumbuka mmoja wa mbinti zake ambaye ana miaka 20 ambaye bado anaamini ni baba yake wa kweli.
Ishii anafikiri wazazi wanapaswa kuwaeleza ukweli watoto wao. ''lakini siwezi kuamua kuhusu hilo,'' anasema kwa masikitiko.