Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Namibu, Kata ya Neruma, Jimbo la Mwibara,Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Lugola amepiga marufuku Makamandawa Polisi wa Mikoa nchini kuyazuia mabasi yanayotoka Mikoa ya Kanda yaZiwa kwenda Dar es a Salaam au kurudi Kanda ya Ziwa muda wa usiku kwa kisingizio cha kuofia kuvamiwa na majambazi. Picha na Wizara yaMambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, (wapili kushoto),akimsalimia Mkazi wa Kijiji cha Namibu, Kata ya Neruma, Jimbo laMwibara, Wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo, wakati alipofanya ziara kijijinihapo. Lugola amepiga marufuku Makamanda wa Polisi wa Mikoa nchinikuyazuia mabasi yanayotoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa kwenda Dar es aSalaam au kurudi Kanda ya Ziwa muda wa usiku kwa kisingizio cha kuofia
kuvamiwa na majambazi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi.
*********************
Na Felix Mwagara, Mwibara (MOHA)
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amepiga marufuku
Makamanda wa Polisi wa Mikoa nchini kuyazuia mabasi yanayotoka Mikoa
ya Kanda ya Ziwa kwenda Dar es a Salaam au kurudi Kanda ya Ziwa
kusafiri muda wa usiku kwa kisingizio cha kuofia kuvamiwa na majambazi.
Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara na kamwe haliwezi kucheka na
majambazi wala kuwaonea huruma majambazi na kuanza kutupangia
majambazi muda gani mabasi yasafiri na yasisafiri, mabasi hayo
yanapaswa kusafiri saa 24.
Akizungumza na katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Namibu Kata ya
Neruma, Jimbo la Mwibara, Wilayani Bunda, Lugola amesema mabasi
yanayosafiri kutoka Kanda ya Ziwa kwenda Dar es Salaam yasizuiwe
Morogoro na yanayotoka Dar es Salaam kwenda kanda ya ziwa yasizuiwe
Shinyanga kwasababu zinazodaiwa za kiusalama.
“Mimi ndiyo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, hatuwezi kupangiwa
ratiba ya kusafiri na majambazi, Serikali ya Rais Magufuli ipo imara, na
Polisi ipo imara, hivyo agizo hili ambalo pia niliwahi kulitoa lizingatiwe
ipasavyo, niliagiza majambazi wote wasambaratishwe, asakwe mpaka
jambazi wa mwisho, akamatwe kama kuku”.Alisema Lugola na kuongeza.
“Taarifa ya uhalifu zinaonyesha Jeshi la Polisi limefanya kazi kubwa ya
kupambana na uhalifu na hasa uhalifu wa majambazi, na niliwahi kuagiza
kipindi hiki si cha kuwa na huruma na majambazi ni kipindi cha
kuwashughulikia ili wananchi waishi kwa amani”.
Lugola alifafanua kuwa, nchi haiwezi kupangiwa na majambazi muda wa
kusafiri, kufanya biashara, hivyo maelekezo aliyoyatoa kwa Jeshi la Polisi
liendelee kupambana na majambazi popote walipo nchini.
“Nimeelekeza magari yanayosafiri yasizuiwe Morogoro yanpopita muda wa
usiku saa nne usiku na kuendelea, yasizuiwe Shinyanga, ili majambzi wajue
popote walipo wapo imara wamejipanga vizuri na mimi Waziri wao nipo
imara kuhakikisha Jeshi la Polisi linawashughulikia makambazi mmoja
baada ya mwingine ili kuwafanya wananchi katika nchi yao waendelee
kushughulika na masuala ya kujijengea uchumi ili Serikali ya Rais Magufuli,
iweze kuwa na uchumi wa kati na majambazi wote wakamatwe kama
kuku,” alisema Lugola.
0 Comments