Jinamizi la muziki wa Ngoma Africa band limeamua kuwaganda na kuwanyima usingizi washabiki wa muziki barani ulaya ! 


bendi hiyo maarufu ya muziki wa dansi Ngoma Africa band aka FFU-ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki Aliens au
"watoto wa mbwa" ni majina ya utani walibatizwa na washabiki wao,
mzimu huo wa muziki Ngoma Africa band inayoongozwa na kiongozi
wake Ebrahim Makunja almaarufu Kamanda Ras Makunja mkuu wa viumbe
wa ajabu ,kikosi hiko kitatingisha maonyesho makubwa ya muziki kule ughaibuni baadhi tu ya maonyesho hayo ni kama yafatanyo na yote yatakuwa siku za jumamosi 
  
03 August 2018 Inter.Afrika Festival Tuebingen,Germany
https://www.youtube.com/watch?v=oTD5ckMYUtM
10 August 2018 Rebstock Park,Frankfurt ,Germany

bendi hiyo inayodumu katika medani kwa miaka 24 sasa ndio bendi pekee ya kiafrika kufanikiwa kudumu kwa muda mrefu na kuwanasa maefu ya wwashabiki kila kona duniani. "Viumbe wa ajabu" Ngoma Africa Band sasa wanatamba na CD yao mpya "Awamu ya Tano Uwanjani" ambayo ipo katika redio mbali mbali hapa nchini.
usikose kuwasikiliza at www.reverbnation.com/ngomaafricaband


https://www.youtube.com/watch?v=oTD5ckMYUtM