Isabel Toledo, aliyesifika kwa mitindo ya fasheni kwa kubuni gauni iliyovaliwa na Michelle Obama katika siku ya kuapishwa kwa mumewe mwaka 2009, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 59.
Mtindo wake wa fasheni ulikuwa kinyume na ilivyozoweleka kwa wanamitindo wengine, kutokana na kwamba wanalioonyesha fasheni zake walikuwa ni kutoka tabaka mbali mbali. .

''Mimi ni mtu wa fasheni'' ," Toledo aliiambia televisheni ta CNN mwaka 2012, badala yake alijiita "mhandisi".
Mme wake na mshirika wake wa kikazi Ruben Toledo amesema kuwa amefariki kutokana na maraddhi ya saratani ya matiti.
"Wawili hao walikutana walipokuwa shule ya sekondari , Ruben akidai kuwa alimpenda Isabel alipomuona kwa mara ya kwanza . Ilichukua miaka minne kwa Isabel kumkubali Ruben kama mchumba wake na mwaka 1984 wakaoana na walikuwa wakishirikiana kwa karibu kikazi ,ilikuwa ni nadra kutowaona pamoja.
Isabel and Ruben Toledo laughing at an event in 2015Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIsabel na Ruben Toledo wwalikuwa washirika wa ubunifu wa mitindo katika kipindi chao chote cha utu uzima
Kwa mchoro na usanii , Bwana Toledo wamekuwa akibuni mitindo iliyotengenezwa na mkewe, likiwemo gauni lililovaliwa miaka ya 1960 na koti ambavyo Bi Michelle Obama alivaa siku mumewe alipoapishwa rasmi kama rais wa Marekani.
Katika siku ile ya kihitoria Januari 2009, randi ya nguo ya mke wa rais anayeingia madarakani iliibua mjadala , huku baadhi wakisema ina rangi ya kijani, wengine manjano na wengine wakisema rangi yake ni ya dhahabu.
lakini Toledo aliielezea rangi hiyo kama ya kijani cha limao au lemongrass, " rangi ya matumaini makubwa , ambayo ina mwangaza wa jua ", aliliambia gazeti la New York Times.
Michelle and Barack Obama walking through Washington DC at his inauguration in 2009Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMichelle Obama alisema kuwa alitaka kuvaa suti ambayo koti lake linaweza kuondolewa na inayoendana na hali ya hewa ya mwezi Januari
Isabel Toledo alifika katika jimbo la Marekani la New Jersey kutoka Cuba alipokuwa katika umri wa balehe. Alianza ushonaji alipokuwa na umri wa miaka minane.
Alipata mafunzo ya kama mbunifu wa fasheni katika Fashion Institute of Technology na baadae alisomea katika shule ya mitindo ya mavazi ya Parsons , kabla ya kujiunga na mhariri wa taarifa za fasheni Diana Vreeland.
Isabel Toledo with the model Dovanna Pagowska at a photo shoot in Times Square, New York City, in 1987Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIsabel Toledo pamoja na mwanamitindo Dovanna Pagowskakatika picha iliyopigwa 1987
Presentational white space
Toledo walifanya kazi kama mwanamitindo wa kujitegemea, ambapo aliwasilisha kazi zake katika klabu ya usiku ya New York mwaka 1984 na baadae aliendelea kuuza nguo zake katika maduka makubwa ya kifahari katika maduka mbali mbali duniani.
Aliiambia televisheni ya Marekani CNN kuwa anapenda "kuhandisi nguo . Kufanya jambo lifanyike. kuifanya nguo isimame''.
Baadae, aliondoa masharti katika miondoko ya fasheni na kuweka mitindo ya ubunifu wake . Kwa muda mfupi alishika wadhfa wa ukurugenzi wa ubunifu katika jumba la fasheni la Anne Klein kuanzia mwaka 2006 hadi 2007.
Isabel Toledo's collection for Lane Bryant fashion show at the Seagram Building on March 20, 2014 in New York City.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIsoabel Toledo's collection for Lane Byrant in 2014
Mnamo mwaka 2012, salichapisha wasifu wenye kichwa cha habari...Misisi ya mtindo, ulioandikwa na Ruben Toledo ambao ulielezea maisha yao pamoja.
Uamuzi wa Michelle Obama wa kuvaa gauni la fasheni Toledo akatika sherehe za kuapishwa uliashiria enzi mpya.
"Nimekuwa kila mara nikiamini katika fasheni inayowahusisha watu wote - watu wa umri wote, maumbile tofauti na mitindo inaypokubalika ,"Toledo aliliambia jaridamoja la fasheni mwaka . "Lengo langu limekuw ani kubuni mitindo ambayo ni ya watu wa tabaka mbali mbali. Ninapenda mabadiliko.
"Ninapenda kufanya majaribio na kufanya kitu cha thamani. Ninapenda kutojua kitu na halafu kukigundua ."
Isabel Toledo standing next to her plus size designs. displayed on mannequins, for Lane Byrant in 2014Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionIsabel Toledo akiwa amesimama kando ya nguo aliyobuni inayovaliwa na mtu mnene aliyoibuni kwa ajili ya onyesho la mitindo la Lane Byrant mwaka 2014