Kiongozi wa jamii ya Wanyarwanda nchini Msumbiji amepigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu Maputo.
Maafisa wanasema Louis Baziga alikuwa ndani ya gari lake Jumatatu mchana baada ya kuondoka nyumbani kwake Matola wakati alipozuiwa na kulengwa na watu waliojihami kwa bunduki.

Baziga alifahamika kuwa mfuasi wa serikali ya Rwanda na alikuwa mfanyabiashara mkuu aliyeendesha biashara ya maduka na duka la kuuza dawa huko Maputo.
Claude Nikobisanzwe, balozi wa Rwanda nchini Msumbiji Mozambique, ameimbia idhaa ya maziwa makuu ya BBC kwamba waliompiga risasi Baziga, walitoweka kabla ya kutambulika.
"Bwana Baziga alikimbizwa hospitalini lakini ikaarifiwa kwamba ameshafariki alipowasili. Polisi wameanza uchunguzi ; nimapema mno kutuhumu kwanini ameuawawa," Nikobisanzwe amesema.
Hii sio mara ya kwanza Baziga kuwahi kulengwa. Aliponea jaribio la kumuua lililotekelezwa na wakaazi wa kutoka Rwanda nchini humo msumbiji mnamo 2016.
Tangu 1994, mataifa ya kusini mwa Afrika yamewahifadhi maelfu wa raia wa Rwanda - wakimbizi na wahamiaji wa halali.
Inaaminika kwamba zaidi ya watu 5,000 wa kutoka Rwanda wanaishi msumbiji.
Kumeshuhudiwa mauaji katika enoe hilo ya wakosoaji wa chama tawala nchini Rwanda wanaoishi uhamishoni, inatuhumiwa wanaolengwa kwa kupinga utawala uliopo.
Mnamo Oktoba 2012, Théogène Turatsinze, mfanyabiashara nchini Msumbiji na aliyekuwa kiongozi wa zamani wa benki ya maendeleo ya Rwanda alitekwa.
Mwili wake uligunduliwa baadaye ukiwa unaelea baharini maputo.
Mahusiano baina ya Afrika kusini na Rwanda umeathirika baada ya kuuawa kwa aliyekuwa mkuu wa ujasusi Kanali Patrick Karegeya, katika hoteli moja mjini Johannesburg mnamo 2014.
Na mnamo Mei, Camir Nkurunziza, aliyekuwa mlinzi wa kitengo cha ulinzi wa rais, alipigwa risasi mjini Cape Town - polisi wamesema alilengwa katika wizi wa gari.
Louis Baziga ni nani?
Bazigaalihamia nchini Msumbiji kwa miongo kadhaa kufuatia mauaji ya kimbari yaliotokea Rwanda
Alikuwa kiongozi wa jamii ya wanayrwanda wanaoishi uhamishoni na alikuwa na uhusiano wa karibu na ubalozi.
Ni mfanyabiashara maarufu aliyemiliki maduka ya jumla na duka la kuuza dawa mjini Maputo.
Alikuwani mfuasi wa serikali ya Rwanda.
Kifo chake Baziga kimethibitishwa na balozi wa Rwanda nchini Msumbiji Claude Nikobisanzwe.