Rais wa Marekani Donald Trump amesema yuko tayari kukutana na rais wa Iran Hassan Rouhani chini ya makubaliano sahihi.
Maamuzi hayo yanakuja mara baada ya waziri wa mambo ya nje alipofanya ziara fupi bila kutangaza katika mkutano wa matifa makubwa 7 yenye nguvu duniani siku ya jumapili.

Mahusiano kati ya Iran na Marekani yamezidi kuwa mabaya tangu Washington ilipojitoa mwaka jana katika makubaliano ya mwaka 2015 ya kudhibiti matumizi ya nyuklia ya Iran.
Licha ya kwamba, siku ya Jumatatu Trump alisema kwamba ana matumain chanya juu ya matarajio ya mpango mpya wa nyuklia na Iran .
"Iran sio nchi ileile miaka miwili na nusu iliyopita wakati nilipoingia madarakani," aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa G7 akiwa na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron .
"Nina imani kuwa Iran litakuwa taifa zuri... lakini hawapaswi kuwa na silaha za nyuklia," alisema," lazima kuwa lazima wawe wachezaji wazuri kabla hajakubali katika mkutano.
Mapema siku ya jumatatu, bwana Rouhani alisema kuwa yuko tayari kukutana na yeyote kama ataona kuwa itakuwa ni kwa manufaa ya Iran.
"Kama sina uhakika kuwa kuhudhuria mikutano hiyo hakutasaidia kuendeleza nchi yangu au kutatua matatizo ya watu wa nchi basi sitasita kufanya hivyo," alisema.
Trump alitoa hotuba ya kuhitimisha mkutano wa G7- mkutano ulioudhuriwa na viongozi kutoka Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza na Marekani.
Masuala mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na moto wa Amazon , maendeleo ya Ukraine, Libya na Hong Kong.
Chart showing key facts about G7
Wamefikaje hapo?
Trump
Mvutano dhidi ya Iran ulirefushwa kwa sababu Marekani ilijitoa katika mpango wa nyuklia wa mwaka 2015, na kuweka tena vikwazo .
Makubaliano mengine yalikuwa ya Uingereza, Ujerumani, Urusi na Uchina walijaribu kuokoa mpango wa nyuklia.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran Mohammad Javad Zarif alisema kuwa alikuwa na mazungumzo mazuri na washirika wa Ufaransa na Macron, pembeni ya mkutano wa G7 huko Biarritz.
Macron ambaye alichukua jukumu la kujaribu kuokoa makubaliano, alisema kuwa alikuwa amemfahamisha Bw Trump kuhusu mpango wake wa kumualika Bwana Zarif, baada ya majadiliano na maafisa wa Iran ili kutafuta uvumbuzi.
Alisema kuwa anaamini kuwa vigezo vya mkutano kati ya Trump na Rouhani ndani ya siku chache zijazo umechapishwa .
"Hakuna ambacho kimewekwa wazi na bado mambo si shwari, lakini mazungumzo yao yameanza kuonyesha maendeleo fulani," alisema na aliongeza kumwambia Rouhani kuwa "kama utakubali kukutana na Trump nina imani kuwa makubaliano yataafikiwa tu".
Mpango Mpya utafananaje?
Makubaliano ya mwaka 2015 yalihusisha Iran kupunguza kwa matumizi ya nyuklia kutoka miaka 10 mpaka 15 na kurejesha kwa vikwazo.
A handout photo made available through the Iranian Foreign Minister Mohammad Javad Zarif's Twitter account shows Iranian Foreign Minister Mohammad Javad Zarif (L) during a meeting with French President Emmanuel Macron (R) and French Foreign Minister Jean-Yves Le Drian (2-R) on the sidelines of the G7 Summit in BiarritzHaki miliki ya pichaJAVAD ZARIF
Mpango huo uliikataza Iran kutotumia rasilimali zake za nyuklia bila ukaguzi kutoka kimataifa .
Iran alielezea vigezo hivyo kuwa havikubaliki.
Katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana Trump alisema mpango mpya kuwa alikuwa anataka kusiwe na silaha za nyuklia kwa muda mrefu zaidi .
Haijafahamika kama Iran itakubali vigezo hivyo vipya" TV ya Iran iliripoti kupinga kwa mazungumzo hayo kuwa hayataweza kufikia makubaliano bila kunukuu aliyesema.
Kwa sasa Macron alisema kuwa kunahitajika kuhakikisha kuwa Iran haitapata silaza za nyuklia na itaweza kusaidika kiuchumi kama itatekeleza hilo.