Mahakama nchini Uganda imempata mwanaharakati na mwalimu wa chuo kikuu cha Makerere nchini humo Dkt Stella Nyanzi ya unyanyasaji wa mtandaoni.
Dkt. Nyanzi ambaye amekuwa mkosoaji mkubwa wa rais Museveni , alishtakiwa kwa makosa mawili, unyanyasaji wa kimtandao pamoja na mawasiliano ya udhalilishaji rais Yoweri Museveni, na mkewe Janet Museveni pamoja na marehemu mama yake Museveni, Bi Esteri Kokundeka, kupitia ujumbe alioutuma kwenye Facebook.
Hata hivyo ameondolewa mashtaka juu ya mawasiliano ya udhalilishaji.
Akitoa hotuba iliyojaa hamasa baada ya uamuzi huyo kutolewa, Bi Nyanzi ambaye alishambiliwa na wafuasi wake na wanaharakati wengine alisema kuwa kama mama hawezi kulia na kuomba kuwa asifungwe gerezani, kwa ajili ya watoto wake.
Kesi yake iliendelea bila kuwepo mahakamani kwa mawakili wa Bi Nyanzi na hivyo kumuacha akijiwakilisha mwenyewe wakati wa hukumu dhidi yake.
"Ninaweza kujitolea kuukosa umama kwa chochote ninachotaka kukifanya . Nilizaliwa kwa ajli ya harakati hizi. Nitaongea kwa madikteta kwa kila lugha yoyote iwezekanayo ," Dkt Nyanzi alimwambia jaji aliyeongoza kesi yake Gladys Kamashanyu.
Kulingana na sheria za Uganda, kosa la unyanyasaji wa kimtandao huadhibiwa kwa kifungo cha miaka mitatu jela.
Nyanzi aliongeza kuwa angependa sana kupatikana na hatia ya makosa kwasababu ni ukweli alipanga kumtusi rais Museveni.
Nyanzi aliandika ujumbe wa matusi ya nguoni uliomuhusisha rais na marehemu mama yake , ambapo alisema kwamba rais Museveni alikufa wakati alipozaliwa.
Jaji aliuelezea ujumbe wa Facebook alioutuma, ambapo Bi Nyanzi alielezea mara kwa mara sehemu za siri za mama yake museveni ,kuwa ulikuwa ni kinyume cha maadili, usio wa heshma na wa kuchukiza, mchafu na wenye matusi mabaya.
Nyanzi alikuwa amekataa kuomba dhamana na amekuwa katika gereza kuu la Uganda la Luzira kwa miezi minane.
Nchini Uganda Uganda, Bi Nyanzi amekua sura na sauti ya matumizi ya lugha chafu katika upinzani dhidi ya kile anachokiita serekali mbaya.
Haoni haya ya kuandika maneno ambayo wengi wanayaona kama ni ya aibu.
Awali alikamatwa na kuwekwa jela kutokana na ujumbe mwingine wa Facebook ambapo alimuelezea rais kama "makalio". Kesi juu ya mashtaka hayo bado inaendelea.
Nyanzi ni mtafiti wa masuala ya jamiina msomi na kabla ya kuanza kampeni yake ya matusi kupitia kwenye mitandao ya kijamii aliwa ni mwalimu katika chuo kikuu cha umma nchini Uganda cha Makerere.
Mashtaka hayo chini ya ya sheria ya matumizi mabaya ya kompyuta ni jaribio latika utekelezwaji wa sheria ya uhalifu wa mtandaoni inayokosolewa.
Wengi miongoni mwa washukiwa wa unyanyasaji wa mtandaoni , wamekuwa hata hivyo wakishutumiwa kwa kumshambulia rais Museveni.
Hukumu dhidi yake imepangwa kutolewa Ijumaa.
|
0 Comments