Wanawake nchini Saudi Arabia sasa wanaweza kusafiri nje ya nchi bila kusindikizwa na wanaume, limesema agizo la ufalme.
Chini ya sheria mpya iliyotangazwa ijumaa , mwanamke mwenye umri wa miaka zaidi ya 21 anaweza kutuma maombi ya paspoti bila idhini ya mlezi wa kiume.

Watu wazima wote wanaweza sasa kuomba paspoti na kusafiri hatua inayowapatia haki sawa na wanaume.
Agizo hilo la ufalme pia linawapa wanawake haki ya kuwasajili watoto wao wanapojifungua, kufunga ndoa au talaka.
Pia sheria hiyo mpya inazungumzia sheria za ajira ambazo zinapanua fursa kwa wanawake.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, raia wote wana haki ya kufanya kazi bila kukabiliwa na ubaguzi wowote kwa misingi ya jinsia, ulemavu au umri.
Hadi sasa, wanawake wa Saudia wamekuwa wakiomba ruhusa kutoka kwa mwanaume mlezi wa kiume, Mme , baba au ndugu mwingine wa kiume kuomba paspoti at kibali chochote cha kusafiri nje ya nchi.
Wanawake wa Saudi ArabiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanawake wa Saudi Arabia
Mtawala wa Saudia Mwanamfalme Mohammed bin Salman amelegeza masharti katika nchi hiyo kama vile kumzuwia mwanamke kuendesha gari kama sehemu ya juhudi kubwa za kufungua taifa hilo.
Mwaka 2016, alifichua mpango wa kufanya mageuzi ya kiuchumi ifikapo 2030, kwa lengo la kuongeza ushiriki wa wamawake kwa 30% kutoka 22%.
Hata hivyo kumekuwa na kesi kubwa za wanawake wanaotaka uhamiaji katika nchi kama vile Canada, kutokana na madai ya unyanyasaji wa kijinsia wakidai.
Mnamo mwezi January, Canada ilimpa hifadhi ukimbizi msichana Rahaf Mohammed al-Qunun mwenye umri wa miaka 18. Aliikimbia Saudi Arabia na kujaribu kutorokea nchini Australia. Alisababisha hali ya sintofahamu katika chumba cha hoteli iliyopo katika uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Thailand Bangkok, ambako alikuwa akiomba msaada wa kimataifa.
Mashirika ya kimataifa mara kwa mara yamekuwa yakidai kwamba wanawake wanachukuliwa kama raia wa daraja la tatu nchini humo.