Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe Selemani Jafo ametangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi kujiunga na kidato cha tano awamu ya pili.
Zoezi la uchaguzi wa wanafunzi hao waliopangwa kidato cha tano limefanyika kwa kuzingatia jumla ya wanafunzi wavulana 1,861 waliokua wamebaki kwenye uchaguzi wa awamu ya kwanza.
Kati ya wanafunzi 1,861 waliochaguliwa ni wanafunzi 1,674 na wanafunzi 187 wamekosa tahasusi hivyo hawajachaguliwa. Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 178 wamepangiwa tahasusi za Sayansi na Hisabati na 1,496 wamepangiwa Sanaa na Biashara.
" Niwashauri waliokosa nafasi waombe kozi mbalimbali katika vyuo vya elimu ya ufundi vinavyotambulika na NACTE, lakini pia waliochaguliwa wanapaswa kuripoti Septemba 2 hadi 16 mwaka huu watakaochelewa watakua wamepoteza nafasi, " amesema Waziri Jafo.
0 Comments