MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo amemtembelea kijana aitwaye Hamza Ashiraf ambaye hivi karibuni alimsaidia kwa kumsafirisha kutoka nyumbani kwao Bukoba na kumleta jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi juu ya uvimbe wake kwenye paji la uso, ambapo ameridhishwa na maendeleo yake baada ya kufanyiwa upasuaji.

Makonda ametumia wasaha huo kuwashukuru madaktari wote walioshiriki kumfanyia upasuaji na kmwezesha hali yake kurejea kwenye matumaini zaidi tofauti na alivyokuwa mwanzo wakati anamuona.

“Ninapomuona leo Ashiraf akiwa katika hali hii kiukweli siamini macho yangu kwani nilivyomkuta mwanzo wakati nachukua hatua ya haraka ya kumsafirisha kuja kupatiwa matibabu ukweli sasa nikimuona nahisi mabadiliko yake ni kama mbingu na aridhi

hivyo sina budi kuendelea kutoa shukurani zangu kwa madakitari wote,” alisema Makonda.SIKU chache zilizopita kijana Ashiraf akiwa kwao Bukoba, alijitokeza hadharani kwenye baadhi ya mitandao ya kijamii akiomba msaada wa matibabu ya tatizo lake la uvimbe uliojitokeza kwenye eneo la uso wake.

Lakini kwa kudra za Mwenyenzi Mungu,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh.Makonda alijitoa kumsaidia na mara moja akamfanyia utaratibu wa ndege ya kumfikisha jijini Dar es Salama na mara moja akaelekeza apelekwe katika hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya uchunguzi zaidi jambo ambalo tayari limeshafanyika na kwamba siku chache zijazo atafanyiwa upasuaji mkubwa ambao utapelekea sehemu kubwa ya uso wake kutoka.

Taarifa kutoka kwa Dkt Bingwa wa upasuaji wa Macho na masikio Edwin Lyombo, amesema, wakati Ashiraf anatolewa Bukoba tayari alikuwa ameshaanza kufanyiwa matibabu lakini Haya kuwa mazuri.

“Nitoe shukurani nyingi kwa Mh Makonda kwa moyo wake wa kujitolea kama huu, kwani endapo watu wengi Zaidi watapatikana kujitolea hapa nchini kusaidia watu wenye matatizo makubwa kama haya basi uwezokano wa kupunguza Malachi makubwa kama haya utaleta tija,” alisema Lyombo.

Ashiraf yeye ameendelea kutoa shukurani zake kwa Makonda kwa kumwezesha kumfikisha Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

“Niendelee kutoa shukurani zangu kwa Mh Makonda kwa kuendelea kutoa mahitaji yote hadi muda huu ambapo leo naonekana mpya tena.,” alisema Ashiraf