Mtoto Abeer Abdallah ambaye ameibuka  mshindi namba moja  katika mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika jijini Antwerpen nchini Ubelgiji.Pichani akiwa na baadhi ya zawadi zake alizokabidhiwa na waandaji wa mashindano hayo.
{Picha na maelezo kutoka Maganga One Blog.}



Mshindi namba mbili wa mashindano ya kuifadhi Quran Al habib Sudeis akipokea zawadi zake kutoka kwa moja wa majaji huku mzazi wake akimsubiria amuongeze zawadi.Sudeis alishangiliwa na watu wengi kwa uhodari wake wa kusoma Quran ukumbini hapo.

Washindi watatu wakiwa wameketi pamoja kutoka kushoto ni mtoto Kauthar {mshindi nambari 3} anayemfuta katikati ni dada Abeer Abdallah {mshindi 1 wa mashindano hayo} na Al habib Sudeis ambaye alishika nambari 2 katika mashindano hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya majaji.Mashindano hayo yalifanyika leo tarehe 21.09.2019 jijini Antwerpen nchini Ubelgiji.
{Picha na maelezo kutoka Maganga One Blog.}

Msichana ambaye alishika nafasi ya nne kati ya washiriki 28 bidada Kamilia akipokea zawadi yake kutoka kwa mmoja wa majaji wa mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika jijini Antwerpen leo tarehe 29.09.2019.Kamilia akipokea zaadi ya Msahafu na tasbihi baada ya matokeo kutangazwa.

Pichani baadhi ya kina mama waliohudhuria kwenye mashindano ya watoto ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika jijini Antwerpen nchini Ubelgiji wakifuatilia kwa makini usomwaji wa Quran kwa washiriki.Mashindano yalijumuisha watoto wa jinsia zote wapatao 28.

Jaji mkuu wa mashindano ya Quran yaliyofanyika leo shekh Ahmad akifungua mashindano hayo kwa kusoma Quran tukufu kama uzinduzi rasmi wa mashindano hayo yaliyofanyika jijini Antwerpen nchini Ubelgiji. 

Mmoja wa washiriki wa mashindano hayo mtoto Bilaly ndiye aliyekuwa mshiriki wa kwanza kupanda jukwaani kusoma Quran kwa siku ya leo ya tarehe 29.09.2019 jijini Anwterpen nchini Ubelgiji.

Wageni kutoka sehemu mbalimbali katika bara la Ulaya walihudhuria mashindano hayo ya Quran yaliyofanyika jijini Antwerpen nchini Ubelgiji leo tarehe 29.09.2019

Hawa ni baadhi ya washiriki wakiwa tayari wanasubiri majina yao yatajwe ili kila mmoja akasome atakavyoongozwa na majaji{hawapo pichani}.Mashindano hayo yaliyoashirikisha watoto 28 na kupata washindi watatu ambao majina yao yapo juu.

Meza kuu ya Majaji

Mshindi wa mashindano ya kuhifadhi Quran bidada Abeer Abdallah Mungu amuongoze vyema insh'Allah duniani na kesho akhera,Mungu awalipe walimu wake kwa wema wao na wazazi wa mtoto pia insh'Allah.
{Picha zote na maelezo kutoka Maganga One Blog.}