Saudi Arabia imesema kuwa itajibu kupitia hatua madhubuti dhidi ya mashambulizi ya hifadhi zake mbili za mafuta huku ikisisitiza madai kwamba Iran ndio iliohusika.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Saudia Adel al- Jubeir alisema kwamba silaha zilizotumika zilikuwa za Iran na kuapa kutoa matokeo ya uchunguzi kamili.

Iran hatahivyo imekana kutekeleza mashambulio hayo. Mapema afisa mkuu wa kijeshi nchini Iran alisema kwamba Iran ilikuwa tayari kuwaangamiza wachokozi wake baada ya Marekani kutangaza kwamba itayapeleka majeshi yake Saudia.
Waasi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran wamesema kwamba ndio waliotekeleza shambulio hilo la tarehe 14 mwezi Septemba ambalo liliathiri usambazaji wa mafuta kote duniani.
Wasiwasi kati ya Marekani na Iran umezidi tangu rais Donald Trump kujiondoa katika mpango wa kinyuklia wa Iran wa 2015.

Msimamo wa Saudia

Akizungumza na waandishi habari mjini Riyadh , bwana Jubeir alisema kwamba Saudia inawasiliana na washirika wake na itachukua hatua madhubuti baada ya uchunguzi wake kukamilika, bila kutoa maelezo ya hatua itakayochukua.
Alirejelea kwamba mashambulio hayo yaliovilenga visima vyake vya mafuta vya Abqaiq na Khurais yalitoka upande wa kaskazini na sio Yemen, lakini haikutaja eneo la moja kwa moja huku ikitoa wito kwa jmaii ya kimataifa kuchukua msimamo.
''Ufalme huu unatoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua jukumu lake katika kushutumu wale waliotekeleza kitendo hiki na kuchukua msimamo mmoja kuhusu tabia hii mbaya inayotishia uchumi ulimwenguni'', alisema.
Wizara ya ulinzi ya Saudia ilionyesha siku ya Ijumaa kile ilichodai kuwa mabaki ya ndege zisizo na rubani na makombora ikithibitisha kuhusika kwa Iran.
Mabaki ya makombora yaliotumika kushambulia hifadhi za mafuta za Saudia
Marekani pia imeishutumu Iran kwa kuhusika na mashambulio hayo huku maafisa waandamizi ambao majina yao hayakutajwa wakiambia vyombo vya habari kwamba ushahidi huo umeonyesha kwamba mashambulizi hayo yalitoka kusini mwa Iran.
Siku ya Ijumaa waziri wa ulinzi nchini Marekani Esper Mark alisema kwamba Marekani itatuma vikosi vya majeshi,
Lakini haikutoa maelezo zaidi kuhusu idadi yake ili kupiga jeki ulinzi wa angani na ardhini wa taifa hilo.
Rais Trump baadaye alitangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran akilenga banki kuu ya taifa hilo pamoja na mali ya taifa hilo iliopo ughaibuni huku akisisitiza kuwa anajaribu kuepuka vita..
Presentational grey line

Iran: 'Tutawakabili maadui zetu hadi mwisho

Mapema kiongozi wa jeshi la Iran Revolutionary Meja jenerali Hossein Salami, alionya kwamba taifa hilo litawaangamiza mara moja maadui zake.
''Mujihadhari kwamba uchokozi wenu hautavumiliwa . Tutakabiiana na adui yeyote hadi tuhakikishe kwamba tumemuangamiza.
Akizungumza katika hafla hiohio , mkuu wa kitengo cha angani cha jeshi hilo Brigedia Amirali Hajizadeh alisema kwamba Marekani inapswa kujifunza kutokana na kufeli kwake katika siku za nyuma na Kwamba shambulio lolote dhidi ya Iran litajibiwa vikali.
Ramani inayoonyehsa washirika wa pande zote mbili
Presentational white space