Bwana harusi Mr.Kassim akiwasili ukumbini  na mkewe Mrs. Mwantum Kassim muda mfupi baada ya kufunga ndoa.Sherehe za harusi zilifanyika nchini Ubelgiji katika mji wa Antwerpen na kuhudhuriwa na ndugu,jamaa na marafiki.
{Picha na maelezo kutoka Maganga One Blog}
Kwa tabasamu la furaha mke halali wa Mr.Kassim bidada Mwantum akikata keki taratibu huku akishuhudiwa na mumewe,sherehe za harusi zilifanyika jijini Antwerpen nchini Ubelgiji majuma mcahache yaliyopita.
"Nakuvesha pete uwe wangu wa milele mke wangu kipenzi"..Bwana Kassim akimtamkia mkewe maneno mazito huku akiizungusha pete taratibu kidoleni kwa mkewe.Ndoa ilifungwa majuma machache na sherehe za harusi hiyo zikafanyika katika jiji la Antwerpen nchini Ubelgiji.
Shughuli ni watu na watu ndio kama mnavyowaona ilikuwa raha sana

Bi harusi bidada Mwantumu akipata picha na mmoja wa rafiki zake wa Karibu Mrs Leah Joseph

Zawadi na mikono ya pongezi kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki zikiwafikia maharusi Bwana na Bibi Kassim.