Eritrea imekuwa ikielezwa kuwa moja kati ya nchi ambazo zinaelezwa kuwa watu wake wanakosa misingi muhimu ya uhuru wa dini na kisiasa.
Suala hili si la ajabu kutokana na kuwepo kwa utawala wa chama kimoja chini ya raisi Isaias Afwerki ambaye amekuwa madarakani tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa Ethiopia mwaka 1993.
Serikali ilipiga marufuku vyama vya upinzani na vyombo vya habari binafsi, pia iliwafunga wakosoaji wa serikali (baadhi ambao hawajasikika kwa miaka sasa) na kuwasajili jeshini vijana wadogo.
Hali hii iliwafanya mamia ya raia wa Eritrea kuikimbia nchi hiyo, Mwandishi wa BBC ameandika namna ambavyo serikali imekuwa ikiyadhibiti maisha ya watu.
1) Kadi za simu ni gharama
Mtandao wa simu unaomilikiwa na serikali, Eri Tel ndio pekee unaotoa huduma za mawasiliano. Huduma zinazotolewa ni mbaya, na unadhibitiwa vikali na serikali.
Ripoti ya Shirikisho la kimataifa kuhusu masuala ya mawasiliano inasema kupenya kwa huduma za mtandao wa intaneti nchini Eritrea ni juu ya asilimia 1.
Wananchi wanapaswa kujisajili serikalini ili kupata kadi ya simu.
Na hata ukupata kadi, huwezi kuitumia ili kupata mtandao wa intaneti kwa sababu hakuna data.
Watu hulazimika kupata mtandao wa kutomua WiFi, lakini mtandao uko chini sana. Kuingia kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter, watu hutumia mtandao wa VPN (virtual private network) ili kuzuia udhibiti wa serikali.
Kwa kuwa kuna ugumu mkubwa wa kupata kadi za simu, watu bado wanategemea simu za Umma za kulipia kabla ya mazungumzo.
2) Watu hutoa hela ndani ya benki pekee
Serikali imeweka sheria kali kuhusu kiasi cha fedha kinachotolewa na wateja wa benki kutoka kwenye akaunti zao.
Hata kama wana mamilioni ya fedha katika akaunti zao, wanaruhusiwa kutoa kiasi cha dola za Marekani 330 kwa mwezi.
Wafanyabiashara hupendelea kuwa na fedha mkononi kwa kuwa mzunguko wa fedha ni mdogo.
Hakuna mashine za kutoa fedha (ATM) nchini Eritrea .Ikiwa kuna shughuli ya harusi siku za usoni, na wahusika wakihitaji fedha zaidi, huomba barua ya kibali kutoka serikalini kwenda benki , na kuruhusiwa kutoa zaidi ya kiasi kilichowekwa na serikali.
Raia wa Eritrea wamtoa maoni tofauti kuhusu sababu za serikali kuweka vikwazo katika kutoa fedha. Baadhi wanasema nia ya serikali ni ''kujenga tabia za watu wenye kujiwekea akiba na kupambana na gharama za maisha'' wengine wakisema kuwa ''serikali haipendi shughuli za kibiashara. Hivyo kudhibiti mzunguko wa fedha''.
3) Kuna televisheni moja pekee nchini humo.
Eri-Tv ni televisheni pekee iliyo nchini ya serikali ya Eritrea. Ni chombo kinachoisemea serikali, lakini ukiwa na satelaiti unaweza kutazama televisheni nyingine za kimataifa.
Kamati ya kutetea waandishi wa habari (CPJ) inatazama kwa karibu suala la uhuru wa vyombo vya habari nchini Eritrea, ikiitaja kuwa nchi inayodhibiti zaidi uhuru wa vyombo vya habari'', nyuma ya Korea Kaskazini.
Hatahivyo, Waziri wa habari Yemane Meskel anasema kuwa asilimia 91% ya nyumba za watu zina mabeseni ya satelaiti.
Haipatikani tena
4) Vijana wadogo wanataka kuondoka
''Kupata pasi ya kusafiria ni kama ndoto iliyokuwa kweli,'' anasema kijana mmoja.
Lakini anasema vijana hawapewi pasi za kusafiria mpaka baada ya kufuzu mafunzo ya jeshi.
Wengine huhatarisha maisha kwa kufanya safari wakivuta bahari ya Mediterrania ili kufika Ulaya, wengi hufa kutokana na njaa na kiu kwenye jangwa na baharini.
0 Comments