Viongozi wa BAKITA na BAKIZA wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha mashauriano.Kutoka kulia waliosimama mbele ni Bi Mwanahija(Katibu Mtendaji - BAKIZA), Dkt.Muhammed Seif Khatib( Mwenyekiti - BAKIZA),Dkt.Sewangi( Katibu Mtendaji- BAKITA) na Dkt.Samwel( Mwenyekiti - BAKITA) na wajumbe wengine.

..............................................

Viongozi wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA) wamekutana jijini Dar es salaam ili kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu maendeleo ya Lugha ya Kiswahili katika mkutano uliofanyika kwenye ofisi za Baraza la Kiswahili la Taifa, jijini Dar es Salaam huku mambo kadhaa ya mashirikiano yalijadiliwa.

Katika majadiliano hayo Ilisisitizwa mabaraza mawili yafanye kazi kwa karibu ili kusadia watanzania kutumia kiswahili kwa ufasaha na usahihi.

Kikao hicho pia kilikubaliana wajumbe kutoka pande zote za Muungano wawe wajumbe wa Mabaraza yote mawili pi kuwepo na kiungo thabiti ili kurahisisha shughuli za uendelezaji wa lugha ya kiswahili kwa pande zote mbili.

Jambo lingine lilijadiliwa ni pamoja na Maneno mapya ya fani na kitaaluma( Istilahi) zinapoandaliwa kwa ajili ya matumizi ni vyema Mabaraza yote yashirikishwe kwa karibu na kukubaliwa kwa maelewano kutimiza malengo ya kukuza kiswahili kwa mafanikio makubwa.

Wajumbe hao pia walikubaliana kuwa uandaliwe mkutano wa vyama vya Kiswahili vya Tanzania kwa ajili ya kukimarisha Kiswahili na kuleta utangamano wa wadau wa lugha hii adhimu ya Kiswahili