Marekani imepiga marufuku mashirika 28 ya China kwa madai ya kuhusika katika unayanyasi wa kabila la Uighurs katika jimbo la Xinjianga nchini China.
Mashirika hayo sasa yameorodheshwa miongoni mwa yale yaliopigwa marufulku na taifa hillo hatua inayoyazuia kununua bidhaa kutoka kwa makampuni ya Marekani bila idhini ya Washington.

Mashirika hayo yaliolengwa yanashirikisha mashirika ya serikali na kampuni za kiteknolojia zinazoshughulika na vifaa vya ujasusi.
Sio mara ya kwanza Marekani imechukua hatua kama hiyo dhidi ya mashirika ya China.
Mnamo mwezi Mei , utawala wa rais Trump uliiweka kampuni kubwa ya teknolojia Huawei katika orodha jhiyo kutokana na hofu ya kiusalama kuhusu bidhaa zake.
Idara ya biashara imesema kwamba mashirika hayo yanahusika na ukiukaji wa haki za kibinadamu na unyanyasaji.
Mashirika ya haki za kibinadamu Beijing yanasema kwamba mashirika kadhaa yananyanyasa Waislamu wa kabila la Uighurs katika kambi za vizuizi .
China imevitaja vituo hivyo kuwa vya kukabiliana na watu wenye itikadi kali.
Idara hiyo ya biashara imesema katika uamuzi wake siku ya Jumatatu kwamba mashirika hayo 28 yanahusika katika kampeni ya China ya ukandamizaji , kuwakamata na kuwazuia watu kadhaa na ujasusi wa hali ya juu dhidi ya Uighurs, Kazaks pamoja na makundi mengine ya Waislamu walio wachache.
Shirika la usalama wa umma la Xinjiang pia lipo katika orodha hiyo pamoja na mashirika mengine 19 madogo madogo.
Kampuni za Hikvision, Dahua Technology na Megvii ni miongoni mwa mashirika manane ya kibiashara yaliopo katika orodha hiyo , yote ambayo yanaangazia utambuzi wa sura ya mtu.
Hikvision ni mojawapo ya kampuni ilio na vifaa vikubwa vya uchunguzi duniani.
Kamera ya HikvisionHaki miliki ya pichaAFP
Image captionHikvision ni kampuni inayoshughulikia vifaa vya Ujasusi
Marekani na China zipo katikati ya mgogoro wa kibiashara na zimetuma ujumbe Washington kwa mkutano kuhusu wasiwasi uliopo kati yao wiki iliopita.
Presentational grey line
Marufuku hiyo pia inalenga kampuni ya China ya AI stars
Hatua hiyo ya Marekani bila shaka itaathiri maono ya kiteknolojia ya China hata iwapo kwa muda mfupi.
Kampuni ambazo zinalengwa ni baadhi ya kampuni kubwa za teknolojia nchini China - sekta ambayo China inalenga katika siku za usoni.
Hatahivyo Algorithm inayotumika katika mafunzo ya AI kwa sasa hutengezwa na kampuni za Marekani pekee kama vile Intel, Movidius na Nvidia.
Hatahivyo hatua hiyo inaishinikiza Marekani kuanza kujitegemea katika utengenezaji wa bidhaa hizo.
Kwa mfano baada ya Huwawei kuorodheshwa katika orodha hiyo ya Marekani mapema mwaka huu hatua iliomaanisha kwamba kampuni kama vile Google zitahitaji kupata leseni ya kuuza nje kutoka kwa Washinton kabla ya kuuza - kampuni hiyo ya China ilisema kwamba itaanza kutengeza programu zake kuweka katika simu zake.
China pia inaendelea kutengeza programu za Marekani ili kujikimu katika kampuni zake za teknolojia.
Huku vita vya kibiashara kati ya marekani na China vikiongezeka kuhusu teknolojia, wateja watahitajika kuchagua kuhusu bidhaa zilizotengezwa China na zile zilizotengezwa Marekani.
Presentational grey line

Je hali ikoje Xinjiang?

China imezindua operesheni kubwa ya kiusalama katika jimbo la Xinjiang , katikja miaka ya hivi karibuni.
Makundi ya haki za kibinadamu na Umoja wa mataifa yanasema kwamba China imewazunguka na kuwakamata zaidi ya watu milioni moja wa kabila la Uighurs pamoja na watu wa makabila mengine madogo katika kambi kubwa ambapo wanazuiliwa, nakulazimishwa kukataa Uislamu, kuzungumza lugha ya Mandarin pekee na kutii serikali ya kikomyunisti ya China.
China inasema kwamba watu hao wanashiriki katika mafunzo ya kuwapatia ujuzi ambayo yanawapatia kazi na kuwasaidia kuingiliana na jamii za China kwa lengo la kuzuia ugaidi.
Kumekuwa na pingamizi kali Marekani na China kuhusu vitendo vya China katika jimbo la Xinjiang.
Wiki iliopita , waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani Mike Pompeo alidai kwamba China inawataka raia wake kuabudu serikali na sio Mungu katika mkutano na vyombo vya habari.
Na mwezi Julai zaidi ya mataifa 20 katika baraza la Umoja wa mataifa kuhusu haki za kibinadamu walitia saini barua ya pamoja ikikosoa jinsi China inavyowatesa watu wa kabila la Uighurs.

Je Uighurs ni akina nani?

Watu wa kabila la Uighurs ni Waislamu Waturuki. Ni asilimia 45 ya watu wanaoishi katika jimbo la Xinjiang ; 40% ni watu wa kabila Han Chinese.
China ilichukua udhibti wa eneo hilo 1949 baada ya kuliangamiza jimbo la mashariki mwa Turkestan.
Tangu wakati huo kumekuwa na uhamiaji mkubwa wa watu wa kabila la Han Chinese na watu wa kabila la Uighurs wanahofia mmomonyoko wa utamaduni wao
Xinjiang ni jimbo huru ndani ya China, kama Tibet iliopo kusini mwake.