KUNA madai kuwa, ile ndoa ya staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na mkewe Faima Msenga ‘Fahyma’ imevunjika, Risasi Jumamosi linakupa mchapo.
Awali, alianza Rayvanny kuposti picha yake katika akaunti yake ya Instagram na kusindikiza na maneno yaliyosomeka hivi:
“Mpende ila usimuamini, mpe ila siyo vyote, mtunze ila usimchunge, mpe mwili wako ila usimpe siri zako, hata mkojo ulikuwa soda. Vitamu ndiyo vichungu keep it your mind.”
Kauli hiyo ndiyo iliyodaiwa kukoleza madai ya kuwa wawili hao wameshamwagana hivyo kuibua gumzo kama lote kwenye mitandao ya kijamii hususan Instagram.
Lakini kama hiyo haitoshi, wakati mambo yakizidi kukorogeka, ghafla Fahyma naye akaposti picha kwenye akaunti yake na kuandika; “Single mama.”
Hapo ndipo mambo yalipozidi kupamba moto na kuwafanya watu waamini kuwa huenda ni kweli wawili hao hawapo tena pamoja.
Baadaye Rayvanny aliandika tena kwenye ukurasa wake akimtakia safari njema mzazi mwenzake huyo huku akimtaka aache kujiita ‘Single mama’.
“Safari njema, lakini badilisha hilo jina.”
Risasi Jumamosi lilimtafuta Fahyma ili kutaka kumsikia anazungumziaje madai hayo ya ndoa yao kuvunjika na hasa kutokana na uzito wa maneno yake aliyoyaandika Instagram ambapo alipopatikana alisema maelezo yake hayahusiani na uhalisia wa maisha yao.
“Ni caption (maelezo ya picha) tu na haihusiani na mambo yetu binafsi,” alisema.
Mrembo huyo alisema kuwa aliamua kuandika maneno hayo katika akaunti yake kwa sababu zake binafsi ambazo hazihusiani na kitu ambacho watu wengi wamekifikiria.
“Niliandika ndiyo, lakini ni posti tu kama posti zingine na haihusiani kabisa na maisha yangu binafsi na mimi na mwenzangu tupo sawa hakuna tatizo lolote,” alisema Fahyma.
STORI: MEMORISE RICHARD
0 Comments