Uganda imezindua simu ya mkononi ya kwanza iliyotengenezwa katika taifa hilo pamoja na kuzindua kiwanda kilichotengeneza.
Kiwanda cha simu nchini Uganda kipo maeneo ya Namanve, mashariki mwa mji mkuu wa Kampala, na kinaendeshwa na kampuni ya China ya ENGO kinachotengeneza simu zinazoitwa SIMI.

Simu za kwanza kutengenezwa katika kiwanda cha nchini Uganda: Kila siku Uganda itatengeneza simu 2000 zitakuwa za kawaida, simu 1500 zitakuwa 'simu za smartphone' na komputa mpakato 800.
'Smartphone' zitauzwa kwa kiasi cha dola 54 na simu ya kawaida ni dola 8.
Simu
Image captionSimu zinazotengenezwa Uganda
Kuanzishwa kwa kiwanda hicho kumetoa fursa kwa serikali ya Uganda kutoa mwanya wa ajira, huku uwekezaji mkubwa ukiwa unatoka China.
Mwaka jana, Uganda ilipokea simu zenye thamani za bilioni moja kutoka China, Huku simu zilizotumwa kwenda China ziligharimu dola milioni 32 kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa mataifa.
China inaongoza pia kwa kutoa misaada katika miundo mbinu ya miradi mikubwa nchini Uganda na mataifa mengine ya Afrika Mashariki.
kampuni ya simu
Kiwanda cha simu,Uganda
Image captionKiwanda cha simu,Uganda