Mshindi wa tuzo ya kimataifa ya uhuru wa habari mwaka jana bwana Maxence Melo, hakuwahi kufikiria kuwa mwandishi wa habari .
Miaka 16 iliyopita ,bwana Melo alikuwa miongoni mwa wa waasisi wa mtandao wa Jamii Forum, mtandao uliokuwa ukiibua masuala ya rushwa na kusaidia kushinikiza uwajibikaji wa viongozi wa kisiasa.

Shughuli hizo zilimpelekea kufahamika duniani, kwa kuwakilisha uandishi bora katika jamii.
Lakini katika miaka mitatu iliyopita, bwana Melo amekuwa mahakamani mara 137 na kushikiliwa polisi mara kadhaa kutokana na kazi yake.
Kazi hii ya uandishi wa habari si safari ambayo imekuwa rahisi kwake: "Inachosha kiukweli, inachosha sana na kuna wakati ninahisi nataka kukata tamaa" aliiambia BBC mwezi Desemba.
Bwana Mello alipata taaluma ya kuwa mhandisi lakini kwa bahati mbaya anajiita mwandishi sasa.
Alianza uandishi wa habari wa kijamii katika tovuti ya Jamii Forum mwaka 2003, tovuti ambayo inawaruhusu wananchi kujadili kwa uhuru masuala yanayohusu taifa lao.
Maxence Melo after he was released from custody in Dar es Salaam 2016Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Tovuti hiyo ilipata umaarufu mkubwa na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa kufikisha ujumbe ingawa misioni yake ilionekana kuichukiza serikali.
Mwaka 2008, bwana Mello alishtakiwa kwa madai ya ugaidi ingawa mashitak hayo yaliondolewa. Lakini haikuishia hapo.
Miaka saba baadae, Tanzania ilipitisha sheria tata ya makosa ya makosa ya kimatandao.
Sheria ya Makosa ya mitandao iliyoanza kufanya kazi mwaka 2015 inamchukulia hatua yeyote atakayechapisha taarifa za uongo au zinazopotosha au ambazo hazijakamilika atakabiliwa na adhabu ikiwemo kifungo au kutozwa faini.
Jamii Forums ilipinga sheria hiyo kwa kuipeleka kesi mahakamani.
Vyombo vya habari, wanahabari na wadau wengine wa habari, sheria hii ilionekana kuwa na nia ya kumunya utendaji wao wa kazi.
Jukwaa la wahariri Tanzania mwaka 2018, lilsema kuwa magazeti matano na radio mbili zilifungwa kwa kipindi cha miezi mitatu miezi 36.
Mwandishi wa habari wa kujitegemea Erick Kabendera alishtakiwa Julai 2019, ili kuhojiwa uraia wake kesi ambayo baadae ilibadilika na kuwa kesi ya uhujumu uchumi.
Kesi yake imekuwa ikihairishwa mara kadhaa kuikilizwa na amekuwa kizuizini tangu wakati huo mpaka sasa.
Tito Magoti, 26, pia ni mwandishi ambaye yupo rumande tangu tarehe 20 Desemba.
Mwaka 2016, aliwahi kushtakiwa kwa kesi ya makosa ya kimtandao. Alishutumiwa kwa kuzuia uchunguzi wakati alipotakiwa kukabidhi taarifa za watu wanaoandika katika mtandao wake.
'Tuna mawakili 18'
Jamii Forums iliwahi kufungwa kwa muda wa siku 21 mwaka 2018, wakilazimishwa kufuata sheria mpya ya maudhui ya mtandaoni.
Licha ya kuadhibiwa na mamlaka na kufikishwa katika vyombo vya sheria, Bwana Melo amekuwa akikumbana na vitisho kadhaa lakini pia alionekana kuwa mshindi.
Mhandisi Melo anayejiita "accidental journalist" (mwandishi wa habari kwa bahati)Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMhandisi Melo anayejiita "accidental journalist" (mwandishi wa habari kwa bahati)
Bwana Mello aliiambia bbc kuwa tangu wafungiwe mwaka jana, waliamua kuwa na mawakili wengi ili kupitia sheria za kimtandao kabla hawajachapisha.
"Tuna kundi la mawakili 18, tulifikiri na kushauriwa namna nzuri ya kufanya kazi yetu na chuo kikuu cha Stanford," alisema.
Lakini bado watu hawana uhuru wa kuongea.
"Awali watu walikuwa huru kuongea, na tulikuwa tunahariri kidogo maoni yao kabla ya kuchapisha katika mtandao wa Jamii forum.
"Ilikuwa unaeza kumpigia mtu azungumzie jambo fulani , awe raia au mwanasiasa. Lakini sasa uwezekano huo ni mgumu au haupo kabisa," aliiambia BBC.

Uhuru wa habari umeshuka

Iliwabidi kupata mawakili kwa ajili ya vyanzo vyao vya habari ili kuwahakikishia usalama wao, ili wasishtakiwe kwa kutoa maoni.
Aliongeza kusema kuwa kwa sasa vyombo vya habari au uhuru wa habari umeshuka Tanzania.
Mwaka jana ' World Press Freedom Index ' iliyochapishwa na waandishi wasiokuwa na mipaka (RSF), walisema kuwa Tanzania imeshuka kwa nafasi 25 s - katika nchi 118 duniani.
"Hakuna taifa lingine ambalo limepitia mabadiliko ya ghafla namna hiyo kama Tanzania kwa miaka minne iliyopita," alisema mkuu wa waandishi bila mipaka.
Aidha serikali ya Tanzania imekuwa ikisisitiza kuwa nchi yake ina uhuru wa kujieleza na kudai kuwa waandishi wa habari wako huru kufanya kazi yao.
Presentational grey line
Presentational grey line
Mkurugenzi wa Jamii Forums amesema kuwa shughuli zake za kila siku, sasa inamlazimu kuwa makini zaidi katika uchapishaji kwa sababu wanaangalia kazi yake kwa karibu
Aidha ana hofu kwa kile ambacho kitatokea kwa siku zijazo kwa sababu Tanzania inaelekea uchaguzi mwaka huu.
"Ni changamoto kweli kwetu sisi... kila mtu ana hofu nini ambacho kinaweza kutokea katika uchaguzi ujao."
Tanzanian President John MagufuliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRais John Magufuli
Bwana Melo anaamini kuwa mamlaka inasikia kilio chao.
"Serikali inaweza kukusukuma kwa nguvu na unapaswa kutafuta mbinu ya kufanya kazi yako kwa ueledi."
Vilevile aliitaka serikali ya sasa kushirikiana na vyombo vya habari ili kupambana na adui rushwa.
"Rais Magufuli ni rais anayeaminiwa na kila mtu kuwa anapambana na rushwa… Ninaamini kuwa kama amedhamiria mapambano hayo ya rushwa, anapaswa kuungana na wadau wa habari."