Marekani imesema iko "tayari kujadiliana na Iran bila masharti" baada uhasama uliozuka baina ya nchi hizo kufuatia mauaji ya jenerali Qasim Soleimani.
Katika waraka wake kwa Umoja wa Mataifa, Marekani ilijitetea kuwa ilimuua jenerali wa jeshi la Iran Qasem Soleimani kama hatua ya kujilinda

Iran ilijibu hatua hiyo kwa kushambulia kwa makombora kambi ya majeshi ya Marekani nchini Iraq japo hakuna mtu aliyejeruhiwa.
Jenerali Soleimani ilichukuliwa kuwa afisa wa pili wa ngazi ya juu nchini Iran.
Kama mkuu wa kikosi maalum cha Quds Force, katika jeshi la ulinzi la Revolutionary Guards' alilikuwa mtekelezaji wasera za Iran katika eneo la mashariki ya kati.
Kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Khamenei amesema shambulio hilo lilikuwa "kofi la usoni" kwa Marekani na kutoa wito kwa nchi hiyo kuondoka mashariki ya kati.
Shambulio dhidi ya Soleimani pia liliwaua wanachama wa kundi la waasi wanaounga mkono Iran ambao pia wamesema watalipiza kisasi.
Hatahivyo, makamu wa rais wa Marekani Mike Pence ameimbia kituo cha habari cha CBS kwamba "ujaususi" unaashiria kuwa Iran imewaambia waaasi hao ambao ni washirika wake wasishambulie ngome zozote za Marekani.
"Tunapokea taarifa za ujasusi za kutia moyo kwamba Iran inatuma ujumbe kwa baadhi ya waasi kutoshambulia ngome za Marekani ama raia, na tunatarajia wataendelea kutoa ujumbe huo," Bw Pence aliambia kituo hicho.
Bunge la wawakili baadae leo Alhamisi linajiandaa kudhibiti uwezo wa rais Donald Trump kuanziwa vita dhidi ya Iran bila idhi maalum kutoka kwa Congress.
Donald TrumpHaki miliki ya pichaEPA
Image captionAwali Rais wa Marekani Donald Trump alisema Iran "inaonekana kurudi nyuma"baada ya kufyatua makombora dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq.

Barua hiyo imesema nini?

Katika barua iliyotumwa kwa baraza lausalama la Umoja wa mataifa, balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa Kelly Craft alisema Marekani iki tayari kufanya mazungumzo na Iran "kwa lengo la kuzuia hatari itakayoathiti amani na usalama wa kimataifa".
Mauaji wa Soleimani yalistahili, barua hiyo ilisema, chini ya kifungu nambari 51 ya sheria ya umoja wa mataifa, inailazimu nchi "kuripoti mara moja" kwa baraza la usalama hatua yoyote ambayo imechukua katika haki ya kujilinda.
Awali Rais wa Marekani Donald Trump alisema Iran "inaonekana kurudi nyuma"baada ya kufyatua makombora dhidi ya kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq.
Bw.Trump, alisema kuwa hakuna raia wa Iraq au Marekani aliyeuawa katika shambulio hilo japo kambi hizo ziliharibiwa kidogo.
Kambi za kijeshi za Irbil na Al Asad zilishambuliwa mapema Jumatano alfajiri.
Iran ilisema ilichukua hatua hiyo kulipiza kisasi mauaji ya wiki iliyopita ya jenerali wake wa ngazi ya juu Qasem Soleimani.
Ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani ililenga msafara wake akiwa na maafisa wa wakuu wa kundi la waasi wanaoungwa mkono na Iran,mjini Baghdad katika hatua ambayo ilizorotesha uhusiano kati ya Iran na Marekani.
Tazama Iran ilivyoshambulia kambi za majeshi ya Marekani
Trump alisema nini siku ya Jumatano?
Rais aliwahi kutishia hatua ya kijeshi dhidi ya Iran ikiwashambulia maafisa wake au kambi yao, lakini hakutangaza hatua yoyote ya kijeshi, akisema kuwa shambulio la Iran halikusababisha majeruhi yoyote.
"Hakuna Mmarekani yeyote aliyejeruhiwa katika shambulio lililofanywa na utawala wa Iran, usiku wa kuamkia jana ," alisema.
"Iran inaonekana kurudi nyuma, hatua ambayo ni nzuri kwa pande zote husika," aliongeza.
Pia alisema kwamba "Marekani ina uwezo mkubwa kijeshi na kiuchumi, hali ambayo inaifanya kuheshimika". "Japo tuna zana za kijeshi za kisasa na zilizo na uwezo mkubwa wa kivita, haimaanishi lazima tuzitumie."
Mabaki ya makombora ya Iran karibu na mji wa al-Baghdadi - Januari 8Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMabaki ya makombora ya Iran karibu na mji wa al-Baghdadi
Bw. Trump pia alisema Marekani itawekea vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Iran, hadi "itakapobadili tabia yake".
"Iran lazima iachane na azma yake ya nyuklia na kukomesha ufadhili dhidi ya ugaidi," alisema.
"Ulimwengu uliostaaarabika lazima utume ujumbe wa pamoja kwa utawala wa Iran. Kampeini yenu ya ugaidi, mauaji na ghasia haitakubaliwa tena na mtu yeyote. Haitakubaliwa kuendelea mbele."
Presentational grey line
Je nini kilifanyika katika shambulio la makombora?
Jumla ya makombora 16 yalifyatuliwa kutoka karibu maeneo matatu nchini Iran, waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper alisema.
Karibu 11 kati ya hizo zililenga kambi ya kijeshi ya Al Asad, magharibi mwa Baghdad, na nyingine moja iligonga kambi ya Irbil,alisema.
Makombora mengine kadhaa yalidondoka hatua kadhaa karibu na maeneo yaliyolengwa.
Shambulio hilo lilifabyika saa nane za usiku majira ya Iran siku ya Jumatano (22:30 GMT siku ya Jumanne).
Wataalamu wa masuala ya ulizi wa Marekani wanaamini tahadhari ya mapema kutoka kwa mifumo yao iliepusha majeruhi.