MECHI ya Watani wa Jadi, Simba Sc na Yanga Sc imemalizika huku timu zote zikitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya mabao mawili kwa mawili.Simba Sc ndiyo ilikuwa timu ya kwanza kupata bao kwa mkwaju wa penati kupitia kwa Medie Kagere dakika ya 42 baada kushikiliwa na Kelvin Yondani ndani ya boksi, bao ambalo limedumu kwa kipindi chote cha kwanza.

Mara tu baada ya Kipindi cha pili kuanza, dakika ya 46 tu Deo Kanda akaiandikia Simba goli la pili, hali ambayo iliwalazimu Yanga kufunguka na kusaka bao kwa udi na uvumba na kufanya comeback ya aina yake.Dakika nne tu baadaye, Mapinduzi Balama akaiandikia Yanga bao la kwanza kunako dakika ya 50, huku Mohammed Banka akiiandikia yanga bao la pili na la kusawadhisha kunako dakika 53.