Uchambuzi wa kina na historia ya mitindo ya Karate chini ya wanzilishi, matawi yake duniani na hatimae kuwa na ushirika na makao makuu huko Japan, ni swala linalohitaji tafakari yenye kina kirefu kwa nia ya kuongoza wafuasi wa vyama tofauti chini ya jina la mtindo mmoja, lakini vyama visivyo na ushirika, au “Affilition”. Nakala hii imenuwia kuelimisha wale wote wapenda Karate, lakini hawana upeo wa kuweza tofautisha nembo

zinazobandikwa katika sare za Karate au “Karate Gi”, ikiwa ni kitambulisho kinachoonyesha kwamba, wewe ni mfuasi wa chama flani ambacho kina ushirika na wale wote wanao vaa hiyo nembo duniani kote. Katika Makala hii, pia tutaweza kuona nembo za mitindo au
mtindo mmoja na kutofautishwa tu kwa vyama .
Hii ni muhimu hasa kwa wafuasi wa Karate wanaotaka kuwa na elimu ya Sanaa hiyo, na kuwa na weledi wa kutambua kwamba huwezi badili nembo tofauti mara kwa mara na kuendelea na ufundishaji wa mtindo mmoja, kwa mfano, wapo watu wanafanya Karate, lakini wanavaa sare za Tae Kwon Do, na bila
hofu wanasema wanafanya Karate. Hiyo sio kweli, sababu kunatofauti ya Karate na Tae Kwon Do.
Vilevile kuna wana Karate ambao wana mitindo au vyama na nembo zao ndio kitambulisho cha mfumo mzima wa mafunzo na uchezaji wa Kata na mbinu tofauti.
Hivyo, haiwezekani , kwa mfano uwe na timu ya mpira kama vile Simba na Yanga au timu yeyote Tanzania, na ukawa unavaa sare au jezi ya timu zote wakati wewe sio timu yako unayoiwakilisha,
kwakweli hili ni tatizo kubwa sana kwa watu wasioweza tofautisha hizi ishara za nembo na uwakilishi wake katika ulimwengu wa Karate. Hakuna budi kuyaeleza haya ikiwa moja ya juhudi za kuwaelimisha kizazi kipya cha wana Karate kwamba, lazima ujuwe na kutofautisha, eidha kupitia mitandao ya dunia
nakutafuta ukweli kuhusu chama unachojitolea kimafunzo kama kinakuelimisha na kukupeleka unapo stahili kimafunzo. Huo ndio uhalisia wa Karateka wakweli na pia kuuliza maswali na kujua historia ya kile unacho jifunza ili baadae kuwaelimisha wengine pia.
Okinawa Goju Ryu Karate-Do ni mtindo mkongwe wa Karate toka visiwa vya Okinawa. Goju Ryu ulipewa jina hilo mwaka 1933 na Master Chojun Miyagi huko Naha, Okinawa. Baada ya mwanafunzi wa Master Miyagi aitwae Shinzato Jinan kuulizwa jina la mtindo wake katika maonyesho ya Karate mjini
Kyoto na kumsimulia master wake Chojun Miyagi baada ya Kurudi Okinawa, ndipo Master Miyagi akaupa mtindo wake jina la Goju Ryu, ikimaanisha Ngumu na Laini kwa ushawishi wa mchanganyiko wa
mtindo wa Naha Te toka Okinawa na ile ya Kichina. Hivyo, bora san ana ni muhimu kwa wana Karate wote kutambua historia ya mitindo yao na maana ya nembo zake.
Hapa kuna baadhi ya nembo za Goju Ryu, lakini zinatofautishwa na vyama vya Goju Ryu, kama vile:
Jundokan Karate-Do, ilianzishwa na Master Eiichi Miyazato mwaka 1957 katika kitongoji cha Asato, mjini Naha, Visiwani Okinawa ambako ndipo kwenye chimbuko la Karate. Master Eiichi Miyazato, ndiye
aliyekuwa msaidizi wa Master Chojun Miyagi mwanzilishi wa Okinawa Goju Ryu katika ufundishaji Chuo cha polisi cha Okinawa na pia Gardens Dojo mpaka hapo master Miyagi kufariki mwezi Oktoba 8,
1953.Pia Master miyagi alikuwa na wanafunzi wengi mashuhuri kama vile Seko Master Higa, Gogen
Yamaguchi, Seikichi Toguchi,, Meitoku Yagi, na Tatsuo Shimabuku.
Elimu hii ya kutambua tofauti za nembo ndio ramani pekee ya utambulisho wa chama unachojivunia
katika Karate.
Kwa mfano, hivi karibuni Jundokan Tanzania ilipata ugeni toka Ureno wa Sensei Nuno Rito Cardeira kwa heshima na taadhima, Sensei Fundi Rumadha Shibu-Cho Tanzania 5Dan, alimuomba Sensei Cardeira wakati walipokuwa katika Gasshuku huko Austria, aje wakati wa likizo yake na kusaidia mafunzo chini ya indhini ya mkuu wa Jundokan duniani Master Yoshihiro Miyazato Kacho na hatimae Sensei Nuno alitimiza hayo yote kwa wana Jundokan wa Tanzania sababu hakuna chama kingine tena duniani chenye makkao yake Okinawa kwa jina la Jundokan.
Vilevile, Master Eiichi Miyazato, alianzisha chama ndani ya Jundokan kwa nia ya kuhamasisha ubora wa Karate kwa ulimwengu wa sasa kwa jina la Okinawa Goju Ruu Kyokai, ikimaanisha Okinawa Goju Ryu ya kileo au Modern maana ya “KYOKAI”, lakini sio mtindo au chama baki. Na baada ya umauti wake
mwezi December 11, 1999, baadhi ya vigogo wa Jundokan au Goju Ryu Kyokai walishawishiwa na kutaka kuunganisha chama kingine cha Goju Kai na hapondipo mtoto wa mwanzilishi wa vyama viwili hivyo Master Eiichi Miyazato aitwa Yoshihiro Miyazato alisema yeye hatorudi nyuma na kujiunga na
chama cha mwanzilishi wa mmoja ya wanafunzi wa baba Gogen Yamaguchi kiitwacho Goju Kai. Pia kwamba Ataendeleza mfumo wa kimafunzo na utamaduni wote ule baba yake alifundishwa na Master Chojun Miyagi.
Hapo ndipo mgawanyo wa vyama ulitokea tarehe 23 mwezi Juni mwaka 2004 chama cha Goju Ryu Kyokai kujitenga na Jundokan So Honbu chama kongwe keundelea na falasala ya ufundishaji ndani ya
Dojo kongwe Okinawa nzima, Jundokan Dojo. Pia vyama hivi viwili viligawana nembo ambazo ziliachwa na mwanzilishi wake master Eiichi Miyazato. Master Eiichi Miyazato alikuwa na wanafunzi wengi waliobobea na kufika hadi Dan 10 na hatimaye nao kuwa na vyama vyao vyenye kutambulika
Okinawa na ulimwenguni. Baadhi ya wanafunzi wa Master Eiichi Miyazato wenye vyama vyao au
viongozi maarufu duniani nikama ifuatavyo: Okinawa Goju Ryu Kyokai iliongozwa na Koshin Iha 10 Dan; IOKGF Master Morio Higaonna 10 Dan; Kiichi Nakamoto sensei 10 Dan Ryukyu Dento Kobujutsu;
Teruo Chinen 9 Dan Jundokan Internation; Master Kuniyuki Kai 10 Dan, Nippon Budoin Seibukan; na Sensei Nantambu Camara Bomani , mwanzilishi wa Jundokan Karate Tanzania,nk.
Kwa upande mwingine alichotetea Kancho Yoshihiro Miyazato kwa maslahi ya baba yake, mwanzilishi wa vyama viwili hivyo, Master Eiichi Miyazato ni kuhifadhi maadili yote na utamaduni kama vile Master Chojun Miyagi alivyomfundisha sababu Kyokai kwa sasa wameweka kipaumbele sana katika Karate ya michezo. Chini ya uongozi wa Kancho Miyazato wapo wasaidizi wake wakuu katika dojo ya Jundokan, Asato, Naha, Okinawa kama vile: Master Tetsunosuke Yasuda 10 Dan; Master Tsuneo Kinjo 9 Dan;
Master Tetsu Gima 9 Dan; Master Yurio Nakada 9 Dan;Master Chuck Merriman 9 Dan; na Master Mike Mancuso 9 Dan.
Mfano wa nembo na mitindo kwa ufupi: