Taarifa za kushangaza zilizoonekana kutamatisha Vita ya Pili ya Dunia, kupotea kwa mwanamume aliyeoonekana muovu machoni pa kila mmoja kulingana na gazeti la London Times - zilipokelewa kwa mshutuko mkubwa ambao ungedumu kwa miongo kadhaa.
Saa 9:30 usiku Mei 1, 1945, ikiwa ni miaka 75 iliyopita, redio ya Hamburg iliripoti kwamba muda si muda inatoa tangazo muhimu kwa watu wa Ujeumani," baada ya hapo ikaanza kupeprusha muziki wa Richard Wagner aliyependwa sana na kiongozi wa Wanazi Adolf Hitler, na kufuatiwa na kipande kifupi cha Anton Bruckner.
"Führer wetu, Adolf Hitler, amekufa mchana wa leo akipigana hadi dakika za mwisho dhidi ya Ubolshevist na kwa Ujerumani," alisema mtangazaji saa 10:20 usiku kabla ya kumpisha mkuu wa jeshi la wanamaji nchini Ujerumani Karl Dönitz, ambaye alidai kwamba kiongozi wa Wanazi amekufa kifo cha kishujaa na pia alikuwa amemtambua yeye kama mrithi wake.
Taarifa hiyo rsami ilizua maswali mengi na wasiwasi mkubwa.
"Wanazi walitumia uwongo kama sehemu ya sera yao, na taarifa za waliokuwa kama Hitler zilikuwa zimesambaa kiasi kwamba matangazo hayo yangeacha maswali na wasiwasi kwamba bingwa huyo wa uwongo anajaribu kufanya ulaghai mkubwa akijaribu kujiokoa machoni pa wengi duniani, " gazeti la The New York Times (NYT) lilionya siku iliyofuata katika taarifa yao waliochapisha.
Makala hiyohiyo, ilibaini jinsi wakaazi wa mji wa Weimar Ujerumani na wafungwa waliokaribu na kambi ya Buchenwald walivyohoji taarifa hiyo.
"Wafungwa wa kisiasa wa Ujerumani niliozungumza nao kwa ujumla hawaamini taarifa hiyo. Wanashuku kwamba kuna njama fulani nyuma ya tangazo hilo lililotolewa.
Pia unaweza kusoma:
- Urusi-Poland zaendeleza mgogoro wao kuhusu vita vya pili vya dunia - kunani?
- Wanawake waliotakiwa kuonja chakula cha Hitler
Hitler alikuwa jambazi kiasi kwamba baadhi waliamini hawezi kufa, "mchambuzi alisema.
Vifo vingi vya Führer (Hitler)
Eneo la Ujerumani lililokaliwa na Muungano wa Usovieti, kukawa na simulizi nyingi za kilichotokea. Zimulizi hizo zikabadilika na kuwa zenye kukinzana.
Mei 3, 1945, jeshi jekundu likaripoti kwamba Hans Fritzsche, Waziri wa ngazi ya pili wa propaganda za Wanazi , Joseph Goebbels, alisema kuwa yeye na Hitler walijiuwa katika makao makuu ya Wizara ya Afya mjini Berlin.
Siku hiyohiyo, stesheni moja ya redio Paris ikadai kupata taarifa kuwa Führer Hitler, alikuwa ameuawa usiku wa April 21, baada ya mzozo na majenerali wenzake kuhusu ushauri wa kuendeleza vita.
Shirika la Habari la Japani la Domei likaripoti kwamba amekufa wakati wa uvamizi wa makombora na muungano wa Usovieti katika makazi yake.
Taarifa kutoka shirika la habari la the UP likaangazia aliyekuwa afisa mkuu wa mambo ya nje wa Wanazi aliyeamini kwamba Hitler amekufa kwa kuvuja damu katika ubongo kwa siku kadhaa na alikuwa amepelekwa mji mkuu wa Ujerumani kufa kama shujaa.
"Nakupa hakikisho kwamba mwili wa Hitler hautatambulika," alitabiri.
Juhudi za kutafuta maiti yake hazikufua dafu.
Mei 4, chombo cha habari cha Muungano wa Usovieti kiliashiria kwamba Jeshi jekundu lilishindwa kuingia katika makao makuu ya serikali ya Ujerumani - kulikokuwa na ofisi za Hitler kwasababu zilikuwa zinaungua na mjengo wenyewe unakaribia kuanguka.
Siku mbili baadaye, Muungano wa Usovieti ulidai kwamba wamepata miili chungu nzima katika ofisi za serikali lakini hakuna mwili ambao walikubaliana ulikuwa wa Hitler au Goebbels.
"Ikaaminika miongoni mwa Warusi kwamba taarifa za kifo chake ni njama nyengine ya Wanazi na kuwa Hitler na wapendwa wake bado wako hai na buheri wa afya," shirika la habari la AP kutoka Moscow likasema.
Mei 8, jenerali wa Urusi akatangaza kubainika kwa mwili uliopigwa risasi katika makumbusho ya Berlin uliotambulika kama Hitler na watu wake wa nyumbani ingawa dereva alidai kwamba huo ulikuwa mwili wa mmoja wa wapishi wake ambaye pia alikuwa mtu wa karibu wa Führer .
Wiki mbili baadaye, Kitengo cha ujasusi cha muungano wa Usovieti kikabaini kwamba kulingana na wafanyakazi wa Hitler, Mei mosi, alitiliwa dawa ya kufa na daktari mmoja kwa jina Morel kwasababu alikuwa amepooza upande mmoja na kupitia maumivu makali sana.
Kutoka Berlin hadi Argentina
Juni 1945, mamlaka ya usovieti ikatoa taarifa kwamba mabaki ya Hitler yamepatikana na huenda bado yuko hai.
Wakati huohuo, taarifa zinakaanza kusambaa kwamba kiongozi huyo wa Wanazi ameonekana katika maeneo mbalimbali akiwa mbali kabisa na wengine.
"Alisemekana kwamba amejitenga katika pango moja karibu na ziwa
Garda kaskazini mwa Italia. Taarifa nyengine ikasema alikuwa mchungaji
milima ya Alps ya Uswisi. Taarifa nyengine zikasema, alikuwa anafanyakazi katika casino ya Evian, Ufaransa. Alionekana Grenoble, huko St. Gallen (Switzerland) na hata pwani ya Ireland, "waliandika wanahistoria Ada Petrova na Peter Watson katika kitabu cha" Hitler's Death ".
Mamlaka ya Marekani, Julai 1945, ikaandika barua inayodai kwamba Hitler anaishi kwenye mashamba huko Argentina, kilomita 700 kuoka mji wa Buenos Aires. Taarifa hizo zilimfikiwa mkuu wa idara ya ujasusi FBI, Edgar J. Hoover, ambaye alitupilia mbali taarifa hizo.
Mwongo mmoja baadaye, taarifa ya kiongozi wa ofisi ya CIA Venezuela ikasema kwamba vyanzo vya fulani vimewasiliana na aliyekuwa mkuu wajeshi aliyedai kwamba alikutana na Hitler mwezi uliopita Colombia. Taarifa hiyo ilisema kwamba ofisi hiyo ina uwezo wa kuthibitisha taarifa hiyo na kuweka picha ya afisa huyo na aliyesemekana kuwa Hitler.
Uwongo wa Muungano wa USoviet
Lakini nini hasa kilichomtokea Hitler?
Baada ya kufanikiwa kuvamia Berlin Aprili 1945, vikosi vya Usovieti vikachukua udhibiti wa mahali alipokuwa Führer makao makuu ya serikali ya Ujerumani.
Mei 2, wanachama wa keshi la usovieti waliofahamika kama - Smersh - walifunga bustani ya Wizara ya Mambo ya Nje na mahali ambapo mkuu huyo wa nazi alikuwa akiishi tangu Januari wakati ambapo jeshi jekundu lilikuwa linaendelea kupenyeza Poland kwa ajili ya Ujerumani.
Shughuli ya kutafuta maiti ilifanyika kwa usiri mkubwa kulingana na mwanahistoria Anthony Beevor, kiasi kwamba hata Marshal Georgy Zhúkov, komanda wa viksi vya Usovieti aliyetekeleza shambulio huko Berlin, hakuruhusiwa kuingia kwa madai kwamba eneo hilo sio salama.
Mei 5, maafisa walibaini mwili wa Hitler na wenzake, Eva Braun, uliozikwa kwenye shimo lililofungliwa kwa bomu katika bustani ya ofisi.
Miili hiyo ilikuwa imenyunyiziwa petrol na kuungua kiasi. Ilikuwa vigumu kumbaini Hitler, na hivyo punde tu maiti yake ilipopatikana walitoa jino moja na kujaribu kuubaini kupitia meo yake.
Hilo lingefanyika siku chache baadaye, pale muungano wa usovieti ulipombaini Käthe Heusermann, msaidizi daktari wa meno wa Hitler aliyewapa historia ya meno ya na data iliyohitajika na kuthibitisha kwamba kweli alikuwa yeye.
Kutoka kaburi moja hadi jingine
Tangu Muungano wa Usovieti kuthibitisha kifo cha dikteta huyo wa wanazi kuanzia mwanzo, kwanini waliendeleza dhana ya kwamba yuko hai?
"Mkakati wa Stalin, bila shaka ulikuwa ni wa kushirikisha Magharibi na Unazi na kutaka ionekane kana kwamba Waingereza au Wamarekani lazima wawe wanaficha ukweli," Beevor aliandika kwenye itabu chake "Berlin, the Fall of 1945."
Luke Daly-Groves, mwanahistoria katika chuo kikuu cha Leeds, anahukkulia hilo kama hatua ya kisiasa iliyochukuliwa na kiongozi huyo wa kikomunisti.
"Alijua kwamba muungano wa Usovieti umepata mabaki ya Hitler aliposema kwamba huenda alikimbia Uhispania au Argentina. Lakini kusema hivyo, kulisaidia kudhoofisha wapinzani wake wa kisiasa na kuimarisha nafasi yake," Daly-Groves aliandika kwenye jarida la the NewStatesman.
Hatimaye kushindwa kwa Wanazi kulifungua milango ya kuanza kwa Vita Baridi.
Moscow ilikuwa na fursa nzuri ya kutetea upande wao: Walichukua na kudhibiti Berlin kuanzia Mei hadi mwanzo wa Julai 1945, pale eneo ya kukaliwa yalipotambuliwaa.
Aidha, waliwazuilia na kuwashikilia manusura kadhaa kwa miaka mingi, akiwemo mpiga picha msaidizi wa Hitler Heinz Linge; mwenzake Otto Günsch na rubani wake Hans Baur.
Kwa haja yao kubwa ya kutaka kuficha ukweli, walimkamata Käthe Heusermann, msaidizi daktari wa meno aliyesaidia katika shughuli ya kubaini mwili wa Hitler.
Baada ya kutengwa kwa miaka 6 alifungwa kwa makosa ya kujitolea kumtibu meno Führer.
Mabaki ya Hitler bado yako chini ya uangalizi wa kitengo cha Smersh kilichopata mwili wake. Kila mahala alipotembea alibebea majivu yake.
Na hatimae, akazikwa katika msitu wa viungani mwa mji wa Berlin, kisha katika mji wa Rathenow jimbo la Brandenburg na mwisho katika kambi ambayo Wasovieti mwaka 1946 huko Magdeburg, katikati ya mashariki mwa Ujerumani.
Na hadi mwaka 1968 kwa mujibu wa kitabu kilichoandikwa Lev Bezymenski, mwanahabari na ujasusi wa Usovieti aliyeshiriki katika uvamizi wa mwisho huko Berlin, taarifa katika hifadhi ya viti vya kale kuhusu Hitler huk Moscow, pamoja na uchunguzi wa maiti yake, ulipowekwa wazi.
Karibia miaka thelathini baadaye, 2009, wakati huo akiwa mkuu wa hifadhi ya siri za serikali, Vasily Khristoforov ndipo alisema kwamba mabaki ya Hitler yalichomwa 1970 na majivu yake yakatupwa katika mto Biederitz.
Kama anavyoelezea Khristoforov, mabaki ya Hitler yalibadilishwa na kuw amajivu kuzuia kaburi lake lisiwe hekali la Wanazi.
Moscow, hata hivyo, ilihifadhi jino la Hitler pamoja na fuvu lake la kichwa katika makavazi ya taifa.
Ukweli ni upi kati ya sumu na kujifytaua kwa risasi
Taarifa iliyotplewa Novemba 1946 na mwanahistoria Hugh Trevor-Roper, wakati wa Viya ya Pili ya Dunia ilitumika aliyekuwa afisa wa kijasusi wa Uingereza na kusimamia uchunguzi wa kifo cha Hitler, alidai kwamba alijitoa uhai karibia saa 3:30 jioni Aprili 30, 1945, pamoja na Eva Braun, ambaye alikuwa amemuoa siku iliyotangulia.
Alijiua kwa kujifyatua kwa bastola mdomoni huku akiwa amejiweka vidogo vya sianidi, ambayo ni sumu kali sana kwa wanadamu na wanyama.
Taarifa hiyo ilizua maswali na kuhojiwa katika kitabu cha Bezymenski ambacho pia kilitaja kwamba maiti ya Hitler haikuwa na sehemu ya fuvu la kichwa.
Mwanahabri Jean-Christophe Brisard na Lana Parshina, ambao kupitia serikali ya Vladimir Putin kwa kiasi fulani mwaka 2016, waliweza kufikia makavazi ya taifa ya Urusi, pamoja na makavazi ya siri ya kijeshi na polisi kuhusiana na kia hicho, alisema kwamba vipande vilivyopatikana kwenye meno ya Hitler - ambayo yalikuwa chanzo cha kufikiwa kuwa huenda alimeza vidonge vya sumu vya sianidi lakini akahoji ikiwa kweli alijiua.
Katika mahojiano 2018 kwenye gazeti la the Times of Israel, Parshina alisema kwamba kiongozi wa kidini alionesha ishara za kutaabika dakika zake za mwisho, kwahiyo, inawezekanaje kwamba alijiua kwa kutumia mkono wake wa kulia akiw akatika hali kama hiyo.
Taarifa zengine zilipendekeza kwamba alijiua kwa kula sumu kisha akajifyatulia risasi akiwa hekaluni.
Mwanamume aliyeahidi kujenga hekalu ambalo litakuwepo kwa miaka elfu, aliachana na kazi hiyo baada ya kuwa madarakani kwa miaka 12, na kutikisa dunia kwa umwagikaji wa damu na moto, na kuharibu kabisa Ulaya na Ujerumani aliyoiacha ikiwa pia imekaliwa.
0 Comments