Idadi ya wagonjwa wa virusi vya corona kisiwani Zanzibar nchini Tanzania imeongezeka na kufikia 134 baada ya wizara ya afya kisiwani humo kutangaza visa vinane vipya zaidi.
Wagonjwa hao wapya walithibitishwa hapo jana tarehe 6 mwezi 2020.
Kulingana na taarifa iliotolewa na serikali ya kisiwa hicho, Wagonjwa wote ni raia wa Tanzania, 16 wanatoka Unguja 13 wanatoka Pemba.

Wakati huohuo Kenya imetangaza wagonjwa 25 wapya wa Covid-19, na kufanya idadi ya wagonjwa nchini humo kufikia 607 tangu kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuripotiwa tarehe 13 Mwezi Machi.
Wizara ya afya nchini humo imesema kwamba wagonjwa 17 kati yao wanatoka Nairobi, huku eneo la Kajiado na Wajiri yakithibitisha visa viwili viwili kila moja nayo Isiolo, Mombasa na Nakuru zikiripoti kisa kimoja kimoja matawalia.
Zanzibar
Katibu mtendaji katika wizaya ya nchini Kenya Rashid Aman pia alitangaza kwamba wagonjwa saba zaidi wameachiliwa huru baada ya kupona na hivyo kufanya idadi ya waliiopona nchini humo kufikia 197.
Pia alisema kwamba wagonjwa watatu zaidi wamefariki na hivyobasi kuongeza idadi ya waliofariki nchini humo kufikia 29.

Zanzibar

Tukirejea nchini Tanzania ripoti iliotolwa kisiwani Zanzibar imesema kwamba mgonjwa mmoja amefariki na kufanya idadi ya waliofariki kisiwani humo kufikia 32.
Ripoti hiyo pia imesema kwamba idadi ya visa ambavyo vimekuwa vikiripotiwa na jamii pia imepungua kwa kiwango kikubwa katika siku ya nne mfululizo.
virusi vya corona
Image captionVirusi vya corona
Imesema kuwa upimaji wa washukiwa wa virusi vya corona sasa utafanyika katika wilaya.
Hatua hiyo inajiri huku Tanzania bara ikimaliza takriban wiki moja bila kutangaza wagonjwa wapya wa ugonjwa huo.
Wagonjwa wanaendelea kupata matokeo Tanzania
Maafisa wa afya nchini humo wamesema kwamba wanaandaa ripoti kubwa ambayo itajumuisha idadi ya wagonjwa wapya katika eneo la Tanzania bara.
Mara ya mwisho kwa eneo hilo kutangaza idadi mpya ya wagonjwa ilikuwa Jumatano iliopita ambapo wagonjwa 480 walithibitishwa kuambukizwa virusi hivyo.
Hatua hiyo imezua wasiwasi kuhusu jinsi taifa hilo linavyokabiliana na ugonjwa huo.
Kulingana na afisa wa mawasiliano katika idara ya Afya nchini Tanzania Tumaini Haonga, Upimaji wa sampuli unaendelea na matokeo yake yatatangazwa na mamlaka zinazohusika.
coronavirus
Life under lockdown divider
Hatahivyo hakutoa tarehe rasmi ya kutolewwa kwa matokeo hayo.
Akizungumza na chombo cha habari cha The Citizen Tanzania bwana Haonga alisema kwamba wagonjwa wapya wamekuwa wakipatiwa matokeo yao binafsi huku akiongezea kwamba idadi ya jumla ya wagonywa waliothibitishwa itatolewa tu iwapo kuna data ya kutosha ya maambukizi mapya.
Matamshi yake yanajiri siku chache baada ya rais Magufuli kutiliashaka matokeo ya maabara kuu ya taifa hilo akisema maabara hayo yanafaa kuchunguzwa kwa kutoa matokeo yenye makosa.

Wagonjwa watano watoweka Old Town

Tukirejea nchini Kenya Aman alisema kwamba kati ya cisa hivyo 25 mtaa wa Eastleigh umethibitisha visa 9 vipya .
Siku ya JUmatano serikali iliwekea mitaa miwili ya Old town mjini Mombasa na Eastleigh jijini nairo amri ya kutotoka kwa saa 24 baada ya maeneo hayo kuandikisha idadi kubwa ya wagonjwa wapya
Akitoa wito kwa raia kuheshimu masharti ya kukabiliana na virusi bwana Ama n alisema imebainika kwamba wakaazi wa Eastleigh na Old Town wamekuwa wakihamia maeneo mengine. Amesema kwamba hatua hiyo huenda ikasababisha maambukizi kwa watu wengine.
Katika mtaa wa Old Town watu watano waliothibitiswa kuwa na virusi hivyo walitoweka majumbani mwao na familia zao.Gavan wa Momabasa Hassan Joho amesema kwamba usakaji wa wagonjwa hao umeanza.