Mwanaume mmoja mkazi wa Mombasa nchini Kenya anayejishughulisha na udereva wa malori yanayosafirisha mizigo kutoka nchi moja kwenda nyingine (transit), amenusurika kupelekwa ‘karantini’ kwa lazima, baada ya kushukiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya Corona.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, mwanaume huyo alikuwa safarini akipeleka mzigo jijini Kampala, Uganda lakini baada ya kufika kwenye mpaka wa nchi hizo mbili, alilazimishwa kupimwa virusi vya Corona na maafisa wa afya pamoja na askari waliopo mpakani hapo na majibu yalipotoka, alidaiwa kuwa na maambukizi.
“Ilibidi arudishwe chini ya escort ya polisi mpaka Mombasa kwa lengo la kwenda kumuweka karantini kwa lazima,” kilieleza chanzo chetu.
Baada ya kufika Mombasa na taratibu za kutaka kumpeleka karantini kuanza, mwanaume huyo aligoma na kutaka kwanza apimwe tena akitumia maelezo ya Rais Dokta John Pombe Magufuli kwamba watu wengine wanapelekwa karantini kutokana na majibu ya vipimo kukosewa.
“Alipaza sauti akisema hawezi kukubali kupelekwa karantini kwa sababu amemsikia Rais wa Tanzania, Dk. Magufuli akisema kwamba baadhi ya mashine huwa zinatoa majibu ya uongo. Alipomtaja Rais Magufuli, ikabidi wale maafisa wa afya wakubali kumpima tena.
“Ajabu ni kwamba majibu yalipotoka, alikutwa akiwa negative kwa maana ya kwamba hana maambukizi, kila mtu akapigwa na butwaa akiwa ni kama haamini. Ikabidi akapimwe tena kwenye mashine nyingine, bado majibu yakawa ni yaleyale, ikabidi wamuachie.
“Aliporudi mtaani, alisikika akishangilia kwa nguvu na kulitaja jina la Rais Magufuli kwamba amewafumbua macho watu wengi kutokana na ubovu wa vipimo vya Corona na kumshukuru sana kwa kumuokoa kupelekwa karantini kimakosa,” kilihitimisha chanzo chetu.
Na Mwandishi Wetu
0 Comments