Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Colin Powell amekosoa vikali rais Donald Trump kwa jinsi anavyoshughulikia maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi akisema kuwa "amejipinda" kutoaka kwa katiba.
Mfuasi huyo wa chama cha Republican, na afisa wa zamani wa ngazi ya juu katika jeshi la Marekani ni wa hivi punde kumkosoa Bw. Trump, kufuatia vitisho vyake vya kutumia majeshi kuvunja maandamano yanayoendelea nchini humo

Amesema atampigia kura mgombea wa urais wa chama cha Democratic Joe Biden katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.
Rais Trump alijibu kwa kumtaja Powell kuwa mtu aliyepewa "hadhi ya juu kuliko anavyostahili".
Bw. Powell, ambaye ni Mmarekani mweusi wa kwanza kuhudumu kama, amejiunga na orodha ya wakuu wa zanmaniwa ngazi ya juu jesheni kumshambulia rais Trump.
Hatua yake inakuja baada ya maandamano ya kitaifa ya zaidi ya wiki moja kupinga ubaguzi wa rangi na dhulma za polisi dhidi ya wananchi zilizosababishwa na kifo cha Mmarekani mweusi George Floyd mikononi mwa polisi mjini Minneapolis Mei 5.
Siku ya Jumapili , wanachama tisa kati ya 13 wa bara za la jiji laMinneapolis waliahidi mbele ya mamia ya waandamanaji kuwa watavuja kitengo cha polisi cha mji huo na kubuni kingine kipya "mfumo mpya wa wausalama wa umma ambao utahakikishia usalama jamii yetu".
Huku hayo yakijiri, mikakakati ya kiusalama iliyokuwa imewekwa kote nchini Marekani kufuatia maandamano hayo imelegezwa.
Mji wa New York imeondoa agizo la kutoytoka nje iliyokuwa imewekwa kwa wiki moja, huku Bw.Trump akisema kuwa ataagiza kikosi maalimu cha ulinzi wa kitaifa kuanzo kuondoka kaytika mji wa Washington DC.
Colin Powell amesema nini?
Akizungumza na kituo cha habari cha CNN Bwana Powell alisema: "Tuna katiba. Na tunastahili kuifuata. Na Rais ametoka kwenye mkondo wa katiba ."
Akimuashiria Rais Trump, jenerali huyo mtaafu malisema: "Anadanganya kuhusu masuala kadhaa, na kuponyoka kwasababu watu hawamwajibishi ."
Kifo cha Floyd: Wamarekani weusi wasema 'hawako salama'
Bw Powell pia alisema matamshi ya rais yanatia mashakani demokrasia , na kuongeza kuwa uchaguzi wa mwaka huu wa urais: "Bila shaka siwezi kumuunga mkono rais Trump mwaka huu."
Aliongeza kusema: "Niko karibu sana na Joe Biden katika suala la kijamii na kisiasa. Nilifanya naye kazi kwa miaka 35, 40. Na sasa ndiye mgombea, nami nitampigia kura."
Bwana Powell, ambaye anaonekana kama Republican wastani, hakumpigia kura Bw Trump katika kura ya maoni ya 2016.
Katika mahojiano hayo, aliwaunga mkono pia viongozi wa jeshi la Marekani ambao walimkosoa Bwana Trump katika siku za hivi karibuni.
Gen Martin Dempsey, Mwenyekiti wa Pamoja wa Wafanyikazi wakati wa utawala wa Barack Obama, aliiambia ABC siku ya Jumapili kuwa matamshi ya Rais yanaharibu uhusiano kati ya Wamarekani na majeshi.
Naye Waziri wa zamani wa Ulinzi James Mattis, wiki iliyopita alimkosoa Trump kwa kugawanya watu makusudi, akisema kuwa "ameghadhabishwa" na jinsi Bwana Trump anavyoshughulikia maandamano yanayoshuhudiwa nchini humo.
Hatua hiyo imepokelewaje?
Katika mtandao wake wa Twitter, Bwana Trump alisema Colin Powell ni "mtu ambaye alikuwajibika sana kwa kutupeleka kwenye Vita vya Mashariki ya Kati", akiashiria vita vya Ghuba vya mwaka 1990-93 na hatua ya Marekani kuvamia kijeshi Iraq mwaka 2003.
Presentational white space
Bwana Biden pia alitumia Twitter yake kumkosoa Trump kwa jinsi alivyoshughulikia maandamano, na kusema kuwa "ametumia visivyo [maneno kama Rais] kuchochea vurugu, kuleta chuki na mgawanyiko, ana kututenganisha zaidi".
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice ameiambia CBC New kwamba angelipendelea Trump ''aachane kidogo na Twitter" na kufanya mashauriano na Wamarekani.
"Sio kila mtu atakubaliana na Rais, lakini kwa hili, Rais huna budi kusema na kila Mmarekani, na wala sio wale tu wanaokubaliana na wewe," alisema.