Zindzi Mandela, mwana wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela na Winnie Madikizela - Mandela, amefariki kulingana na chombo cha habari cha taifa hilo SABC.
Zindzi amefariki mjini Johannesburg mapema Jumatatu akiwa na umri wa miaka 59.
Kifo chake kimethibitishwa na chanzo kimoja cha familia, kimesema chombo cha habari cha SABC.
Alikuwa balozi wa Afrika Kusini nchini Denmark. Amewaacha watoto wanne na mumewe.

Unaharakati na siasa

Mwanamke huyo alikuwa mwanarakati wa kisiasa na ni miongoni mwa wale waliopigana dhidi ya uongozi wa ubaguzi wa rangi nchini humo.
Alianza kuhudumu kama balozi wa Denmark mwaka 2015.
Alikua mwana wa sita wa Nelson Mandela na wa pili kati yake na Winnie Madikizela Mandela.
Wakati alipokuwa na umri wa mwaka mmoja na miezi sita babake, alifungwa jela. Mamake pia alifungwa mara kwa mara wakati huo.
Mwaka 1977 Madikizela Mandela alipelekwa katika eneo la Brandfort, katika jimbo la Orange Free State na Zindzi aliandamana naye.
Baadaye alielekea nchini Swaziland na alipokamilisha shule ya upili, alijiungana na Chuo kikuu cha Cape Town kwa shahada ya sheria.
Yeye na dadake walianza kuwa wazungumzaji wa wazazi wao waliokuwa wakihudumia kifungo jela.
Zindzi Mandela:
Maelezo ya picha,
Mwana wa kike wa Nelson Mandela, Zindzi aaga dunia
Mwaka 1985, aliofuzu . Zindzi alichaguliwa kusoma taarifa ya babake ya kukataa kutoka jela baada ya aliyekuwa rais wa taifa hilo PW Botha kumtaka kutoka jela bila masharti.
Wakati babake Nelson Mandela alipotoka jela 1990, mazungumzo yalianza kati ya chama cha ANC na utawala uliokuwepo kufutilia mbali mfumo wa ubaguzi wa rangi.
Huku Afya ya aliekuwa rais wa ANC ikizorota , Mandela alichaguliwa kama raia mpya wa Chama cha ANC na mgombea wa urais nchini Afrika kusini katika uchaguzi wa 1994.
Baada ya Mandela kuchaguliwa rais na kumpatia talaka mkewe Winnie 1996, Zindzi alichaguliwa kuandamana na babake katika sherehe ya kumuapisha.