ALIYEKUWA mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joshua Nassari,  ameangukia pua katika kura za maoni jimbo hilo ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushika nafasi ya nne akipata kura 26.

Aliyeibuka mshindi kwenye kura hizo ni mbunge wa sasa anayemaliza muda wake, Dk. John Pallagyo, aliyepata kura 536 akifuatiwa Dan Pallagyo kura 63.