Charles Bukeko maarufu kama 'Papa Shirandula' ameaga dunia katika hospitali ya Karen mjini Nairobi
Charles Bukeko, msanii maarufu nchini Kenya aliyejulikana kwa jina la 'Papa Shirandula' ameaga dunia.
Kulingana na msemaji wa familia Richard Ekhalie, Papa Shirandula ameaga dunia hospitali ya Karen hii leo.
Mchana huu familia ilikuwa inasubiri ripoti maalum kutoka hospitali ili kuthibitisha kilichosababisha kifo cha mpendwa wao.
Papa Shirandula alifikishwa hospitali leo asubuhi saa mbili na nusu na mke wake, akiwa hajisikii vizuri lakini wakati wanajaribu kuendelea na mchakato wa kulazwa hospitalini, Papa Sharandula akaaga dunia.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia, siku ya Jumatano Papa Shirandula alikuwa ametoka kuandaa vipindi kama ilivyo kawaida yake lakini akawa hajisikii vizuri na kupata dawa, lakini leo usiku, hali ikawa bado inaendelea ndio mkewe akamkimbiza hospitali baada ya kuanza kusikia vibaya karibu saa kumi na moja asubuhi.
Papa Shirandula ni nani?
Charles Bukeko maarufu kama Papa Shirandula anatoka magharibi mwa Kenya eneo la Busia.
Ameacha nyuma watoto wawili na mke wake waliokuwa wanaishi mjini Nairobi.
Bukeko ambaye jina la Papa Shirandula limetokana na kipindi kimoja cha anachoshiriki kinachopeperushwa na runinga ya Citizen, amekaa katika tasnia hii ya uigizaji kwa muda sasa na ingawa msemaji wao wa familia Bwana Ekhalie hakuwa na uthibitisho wa ni lini hasa aliingia kwenye uingizaji amesema kwamba sio chini ya miaka kumi.
Mbali na kushiriki kipindi kilichompa umaarufu mkubwa, 'Papa Shirandula' ameshiriki kwenye utengenezaji wa maudhui ya kipindi hicho na kushinda Tuzo la Kalasha Award, 2010 kama muigizaji mzuri kwenye vipindi vya televisheni, pia alikuwa kwenye filamu ya 'The Captain of Nakara' mwaka 2012.
Aidha amehusika na matangazo ya biashara mbalimbali pamoja na kuendeleza kurudumu lake la uigizaji kwenye maonyesho tele aliyoshiriki katika ukumbi wa taifa wa uingizaji Kenya.
Watu wamepokeaje kifo chake.
Ezekiel Mutua Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya udhibiti wa maudhui ya usanii nchini Kenya (KFCB)
Kifo cha Papa Shirandula kimegusa wengi.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya udhibiti wa maudhui ya usanii nchini Kenya (KFCB) Ezekiel Mutua, amemtaja Papa Shirandula kama mtu aliyejitoa na kutumia kipaji chake kufurahisha Wakenya na kuwapa matumaini.
Rest in peace Charles Bukeko alias Papa Shirandula. You were a self-made man who epitomised the joy and optimism of Kenyans. You made a huge contribution to the entertainment industry in Kenya. We will miss you. May God give peace, comfort and strength to your family and fans.— Dr. Ezekiel Mutua, MBS (@EzekielMutua) July 18, 2020
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, amesema kupitia akaunti ya mtandao wa Twitter kuwa Mombasa inaomboleza msanii Bwana Charles Bukeko aka Papa Shirandula na kutoa rambirambi zake.
Mombasa mourns the loss of kenya's renowned creative artist to grace our screens Mr. Charles Bukeko aka Papa Shirandula who passed on this morning at the Karen Hospital. I extend my sincere condolences to his family and friends. May the Almighty rest his soul in eternal peace. pic.twitter.com/v8n3acqWiY— Governor Hassan Joho (@HassanAliJoho) July 18, 2020
Mwisho wa Twitter ujumbe, 2
Mtangazaji mkongwe Fred Obachi Machoka ametuma rambirambi zake kwa familia, marafiki na wasanii wenzake.
Sincere condolences to the family and friends of our colleague and friend the late Charles Bukeko a.k.a. Papa Shirandula. Rest in peace bro. pic.twitter.com/AalhZEjQjv— Fred Obachi Machoka (@fredomachoka) July 18, 2020
Mwisho wa Twitter ujumbe, 3
Kama mwingine yeyote yule, Papa Shirandula alikuwa na uraibu wake, alipenda sana mpira wa sika na timu aliyoishabikia nyumbani ilikuwa AFC Leopards.
TRANSITION— AFC Leopards SC (@AFCLeopards) July 18, 2020
We are sad to learn about the sudden death of our super fan and member Charles Bukeko
Our heartfelt condolences to his family and friends . Our thoughts and prayers are with his family and friends at this trying moment.
Rest In Peace PAPA SHIRANDULA pic.twitter.com/cIZ3tYvGIV
Mwisho wa Twitter ujumbe, 4
Kuna madai kutoka kwa baadhi ya vyombo vya habari kwamba Papa Shirandula huenda amekufa kwa ugonjwa wa virusi vya corona lakini kupitia mazungumzo na BBC Swahili, msemaji wa familia Richard Ekhalie amesema kuwa huko ni kukisia tu.
Aidha msemaji wa familia amethibitisha kwamba wamekuwa na mkutano kidogo na hospitali lakini bado haijatoa taarifa rasmi na sasa hivi familia inapanga mipango ya kupeleka mwili kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
0 Comments