Madai ya kuwa vipimo vya corona vinaweza kusababishia watu madhara, yameenea katika mitandao ya kijamii.
Uchunguzi wa baadhi ya madai hayo ambayo yameshirikishwa katika mitandao ya kijamii.

Kipimo cha puani kinaweza kuharibu ubongo

Picha inayoonyesha mtu akipimwa corona puani 'swab test' imesambaa katika mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram ikiwa na madai kuwa kipimo hicho kinaweza kuleta kizuizi cha damu katika ubongo.
Wazo la kuwa kipimo hicho kinaweza kusababisha kizuizi cha damu katika ubongo, jambo ambalo halikueleweka hata kidogo kuhusu ufanyaji kazi wa kipimo hicho.
Ubongo una sehemu nyingi za kuulinda. Kwanza kabisa, fuvu la kichwa ni ulinzi tosha kwa ubongo na vilevile ubongo unalindwa na majimaji.
Mishipa ya damu ambayo inaenda kwenye ubongo, haiwezi kusababisha kuzuia damu kufika katika ubongo, wakati ikiruhusu vitu kama oksijeni na lishe .
Kipimo hicho cha kijiti cha pamba hakiwezi kuharibu tishu zozote au mfumo ambao upo na kufanya mishipa ishindwe kusukuma damu mpaka kwenye ubongo.
Post on social media claiming that the blood brain barrier is the spot where a coronavirus test using a nasal swab is carried out. We labelled it 'false'. Includes anatomical drawing of swab stick inside a nose.
"Kipimo hicho hakiwezi kufika katika kizuizi cha damu katika ubongo bila ya nguvu kubwa kutumika, maana kuna sehemu kadhaa ambazo zinalinda tishu na mifupa.
Hatujaona madhara yeyote ambayo yanasababishwa na kipimo cha corona tangu tumeanza kufanya vipimo hivi," alisema Dkt Liz Coulthard, mjumbe mtendaji wa 'British Neuroscience Association (BNA)'.
Mbinu ya upimaji wa virusi vya corona kwa kutumia kifaa hicho hakijaonyesha madhara hayo yanayotajwa.
Upatikanaji wa maambukizi kupitia koo na pua unatumiwa Uingereza kupima Covid-19 .
"Nimewapima wagonjwa wangu kwa kutumia mbinu hiyo hospitalini na vilevile kujipima mwenyewe kila wiki pamoja na watu ambao walijitolea kufanya jaribio la upimaji.
Haiwezekani kitu hicho ambacho kinaingizwa kwenye pua kwenda mbali kiasi hicho - unaweza kuhisi kuwashwa lakini hakuna maumivu yoyote," alisema Dkt Tom Wingfield kutoka shule ya tiba ya Liverpool.
Madai hayo ambayo yamejitokeza katika mtandao wa Facebook, katika kurasa za watu watano ambao wanaishi Marekani, Julai 6, madai hayo ni kama yanawataka watu wakatae kupimwa.
Madai hayo ni ya uongo.
Tumeona baadhi ya picha za grafiki ambazo ziko kwa lugha ya kirumi, kifaransa na kireno, huku maelfu ya watu wakiwa wameshiriki kutoa maoni.

Vifaa vya kupimia corona haviwezi kukuambukiza corona

Taarifa zinazoeleza kuwa vifaa vinavyotumika kupima corona vinaweza kukuambukiza corona ni jambo ambalo halina ukweli wowote, huo ni upotoshaji.
Kiukweli, kichwa cha habari kilitafsiriwa ndivyo sivyo, ripoti ambayo iliandikwa mwanzoni mwa mlipuko haikumaanisha ukipima corona basi unakuwa umepata maambukizi.
A Facebook post labeled "misleading" which says "You want covid 19? This is how U get it!" and links to a Washington Post article about contaminated test kits.
Ujumbe huo ulitumwa na zaidi ya watu 3000 kwenye mtandao wa Facebook, kurasa ya mtangazaji wa Fox News Tucker Carlson alituma makala ambayo inaonyesha vipimo vya corona na kusema : "Unataka Covid-19? Unaweza kuipata hivi?"
Makala hiyo ambayo ilichapishwa mwezi Juni, ilisababisha uchelewaji wa watu kufanya vipimo, maana makala hiyo ni kama ilikuwa inaelekeza kuwa mpango wa kituo cha uthibiti magojwa-CDC .
Makala hiyo haikueleza kuwa vipimo vipimo vya corona vinaweza kusababisha watu kuugua corona.
Watu wengi wanaweza kuwa walisoma kichwa cha habari cha makala hiyo badala ya kusoma maudhui yake.
Madai ya uongo yanayohusisha ufadhili wa taasisi ya Gates ambayo yanadai kutoa msaada kwa wagonjwa , yameshirikishwa na maelfu ya watu na kuwekwa mara nyingi katika kurasa ya Facebook yakihusishwa na madai ya chanjo.
Hakuna uthibitisho wowote unaojumuisha mpango wa micro-chipping na mlipuko wa virusi vya corona na Taasisi ya 'Bill and Melinda Gates Foundation' imekanusha madai hayo na kuhusisha na chanjo.
' Kwanini huwezi kupumua kwenye kipimo hicho?'
"Kama kweli Covid 19 inabebwa na hewa , kwa nini mtu asipumulie tu kwenye kipimo hicho? Kwa nini kipimo hicho kiingizwe mpaka ndani ya pua?"ujumbe huo umewekwa mtandaoni mara 7,000 hivi katika mtandao wa Facebook na Instagram.
Two memes we labelled 'misleading' asking "If COVID was really carried on your breath, why can't you just breathe on the swab? Why do they have to shove the swab to the very back of your nose?"
Virusi vya corona vinasambaa kwa mtu pale mtu mwenye maambukizi anapokohoa au kupiga chafya - na kutoa tone ndogondogo za virusi katika hewa.
Hiyo haimaanishi kuwa kupumua tu katika kipimo kunaweza kufanya kukusanya kiasi cha kutosha kwa sampuli ya kupima katika vipimo vya maabara.
Wataalamu wa afya wanasema , kipimo kuingizwa ndani ya pua kunaweza kuleta matokeo sahihi zaidi.
Kama unaweza kupumulia tu kipimo hicho, unaweza usipate vipimo unavyohitaji au seli ambazo zina virusi.
Hata hivyo kama utaweka kipimo ndani ya pua na koo na kukiangazia katika sehemu yenye maambukizi, ni rahisi zaidi kupata taarifa sahihi za matokeo ya kipimo.
Presentational grey line
Vyeti vya uongo vya matokeo ya virusi vya corona, nchini Bangladesh
Mwisho utafiti uliangazia madai ya cheti cha uongo ambacho kilizua gumzo huko Bangladesh baada ya kuelezea mtu kuwa hana virusi vya corona.
Watu kadhaa walikamatwa baada ya kuonyesha vyeti vya uongo vinavyoonyesha hawana maambukizi wakati hata hawajafanya vipimo.
Nakala za vyeti hivyo zimekuwa zikihitajika kwa wafanyakazi wahamiaji kuonyesha kuwa hawana maambukizi ya corona wakati wanapofika katika eneo wanakoenda.
Kipato cha Bangladesh kinategemea raia wa kigeni zaidi.
Katika tukio la hivi karibuni, mmiliki wa hospitali alishutumiwa kwa kufanya vipimo kadhaa vya uongo, alishikiliwa kwa muda wa siku tisa na baadae akapatikana katika mpaka wa India akijifanya mwanamke.
Magenge ya wahalifu pia yanaweka matangazo katika mitandao ya kijamii kupata wateja.