ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Map[induzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, ameshinda kura za maoni za CCM Jimbo la Iringa Mjini kwa kupata kura 190 na kuwabwaga wagombea wengine akiwemo Steve Nyerere aliyepata kura 6.
Matokeo ya kura za maoni katika jimbo hilo ni:
Jesca Msambatavangu – 190
Nguvu Chengula – 75
Ibrahim Ngwada – 44
Steven Mengere (Steve Nyerere) – 6.
“Asante Iringa hakika nimejiona wa thamani sana tulikuwa wagombea  57 mimi nimekuwa mtu wa tisa wengine wote kura moja, wengine zero. Hivi ningekosa kabisa ningeweka wapi sura yangu?  Asante wana Iringa hata hichi kidogo mlichonipa kwangu ni heshima pia.
“Kwanza nichukue nafasi hii kusema asante Mungu kwa kila jambo, hakika nimeona uwezo wako nimeona nguvu yangu nimeona kipaji changu nimeona jinsi gani Baba anavyonipigania kwenye kila jambo, niseme Asanteni sana Wasanii wenzangu mlionikimbilia kwenye hili.
“Asante marafiki zangu Ndugu zangu pamoja na Waandishi wa habari wote nasema bila nyie mimi siwezi, niseme asante kwa Chama changu Viongozi wote wa Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Ally Hapi, Salim Asas, DC Richard Kasesela na Viongozi na Wanachama wote wa CCM.
“Niseme tu kukosa kura sio sababu ya kuacha mapambano nitashirikiana na Mgombea kuhakikisha Jimbo linarudi lakini kikubwa zaidi ni kutafuta ushindi wa hali ya juu wa Chama cha Mapinduzi kuanzia kura za Rais, Mbunge mpaka Diwani.
“Narudia tena asante Iringa hakika nimejiona wa thamani sana tulikuwa Wagombea 57 katika hao wote mimi Steve Nyerere nimekuwa Mtu wa 9, wengine wote kura 1 wengine sifuri, hivi ningekosa kabisa ningeweka wapi sura yangu asante wana Iringa hata hichi kidogo mlichonipa kwangu ni heshima pia,”  alisema Steve Nyerere