Real Madrid inaamini kuwa mshambuliaji Kylian Mbappe ,21, atakuwa na mazungumzo nao kuhusu uhamisho kutoka Paris St-Germain. (Marca)
Chelsea iko tayari kumpatia kipa wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak ofa £90.7m. (AS - in Spanish)
Paris St-Germain inamlenga mshambuliaji wa Manchester United na Marcus Rashford, 22,. (Independent)
Barcelona inamuuza kiungo mchezeshaji wa Brazil Philippe Coutinho, 28, kwa Arsenal na Newcastle huku wakijaribu kutafuta fedha za kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22. (Goal)
Phillipe Coutinho
Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, anataka kurudi Barcelona, na Paris St-Germain wanapiga hesabu za thamani yake huku akiwa amesalia na kandarasi ya miaka miwili katika mkataba wake (Mundo Deportivo - in Spanish)
Kiungo wa kati wa Southampton na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, anataka kujiunga na Tottenham, ambayo inaweza kumtumia beki wa England Kyle Walker-Peters 23,kuafikia. (Evening Standard)
Mshambuliaji wa Lille na Nigeria Victor Osimhen, 21, amechagua kujiunga na Napoli katika mkataba wenye thamani ya Yuro milioni 81m (£73.5m). (RMC Sport - in French)
Mshambuliaji wa Lille na Nigeria Victor Osimhen, 21, amechagua kujiunga na Napoli katika mkataba wenye thamani ya Yuro milioni 81m (£73.5
Maelezo ya picha,
Mshambuliaji wa Lille na Nigeria Victor Osimhen, 21, amechagua kujiunga na Napoli katika mkataba wenye thamani ya Yuro milioni 81m (£73.5
Manchester United itakosa malipo ya £25m kutoka kwa wafadhili iwapo watafeli kufuzu katika michuano ya kombe la klabu bingwa Ulaya. (Daily Mail)
Beki wa Liverpool na Uskochi Andrew Robertson, 26, anavutiwa ba uhamisho lakini atatia kandarasi ya muda mrefu na. (Lockdown Tactics via Express)
Zlatan Ibrahimovic
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 38, amesema hana uhakika kuhusu mustakabali wake ndani ya AC Milan kwa kuwa hakuna mazungumzo yoyote yaliofanyika kuhusu mkataba ikiwa sasa ni chini ya mwezi mmoja kabla ya mkataba wake kufikia ukingoni. (Sky Sports)
Luca Jovic
Kai Havertz anataka kuondoka Bayer Leverkusen kwasababu walishindwa kufuzu katika michuano ya klabu bingwa Ulaya hivyobasi Chelsea watalazimika kuhakikisha wanafuzu katika michuano hiyo ili kumshawishi kiungo huyo wa Ujerumain 21 kujiunga na timu hiyo.. (Bild)
Bayern Munich wanajiandaa kuanza mchakato wa kumnasa Tanguy Ndombele ,23, wa Tottenham na Mfaransa mwenzie anayecheza katika nafasi ya kiungo cha kati katika klabu ya Monaco, Tiemoue Bakayoko,25. (Le 10 Sport via Daily Mail)
Nice imetoa ofa kwa kiungo wa kati Mhispania Rony Lopes anayekipiga Sevilla. (RMC Sport-in French)
Mkurugenzi wa michezo katika klabu ya Norwich Stuart Webber amesema kwamba ombi la kutaka kumnunua mchezaji kinda mwenye kipaji mwisho wa msimu litaanza kwa dau la £20m . (Norwich Evening News)
Mourinho na Tanguy Ndombele
Brentford inamlenga winga wa Portsmouth Ronan Curtis, 24 kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Said Benrahma ikiwa ataondoka kwenye klabu hiyo. (The News, Portsmouth)
Barcelona yakataa uwezekano wa Neymar kurudi katika klabu hiyo
Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amekataa uwezekano wa mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar,28, kurejea Nou Camp lakini amesema klabu inafikiria uhamisho wa mshambuliajji wa Inter Milan Muajentina Laitaro Martinez, 22. (TV3 Mundo Deportivo)
Bartomeu pia amesema ana ''uhakika'' mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi,33, atasalia Nou Camp zaidi ya mwaka ujao. (TV3 via Evening Standard)
Manchester City itatoa ofa kwa kocha Pep Guardiola ya mkataba wa muda muda mrefu baada ya marufuku dhidi ya klabu hiyo kufutwa. (Mirror)
Pep Guardiola
Guardiola atapatiwa karibu kitita cha pauni milioni 150 kwa ajili ya kukipa nguvu kikosi cha City. (Guradian)
Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N'Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili ya kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa, 29. (Gazzetta dello Sport, via Metro)
Zenit St Petersburg wameeleza nia yao ya kumsajili beki anayekipiga katika klabu ya Liverpool Dejan Lovren, 31. (Liverpool Echo)
AC Milan wanafiukiria kumnunua mashambuliaji wa Real Madrid raia wa Serbia Luca Jovic, 22, ambaye anayekodolewa macho na Leicester City na Arsenal. (Calciomercato,via Leicester Mercury)
Bayern Munich wana mpango wa kuwanasa viungo wawili wanaocheza ligi kuu ya Ufaransa, Tonguy Ndombele wa Tottenham, 23, na Tiemoue Bakayoko. (Le 10Sport)
Mashabiki 5,000 waliruhusiwa kuingia uwanjani kutazama mechi ya kirafiki ya Paris St Germain, mechi iliyoitoa kifua mbele kwa 9-0 dhidi ya wenyeji Le Havre. (France 24)