WASHINDI  wa uchaguzi kwenye kura za maoni za ubunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) waliopita kwenye majimbo yao ni kama ifuatavyo:

1.Mshindi Jimbo la Kawe ni Halima Mdee mwenye kura 63 (71.5%).
2. Tarime Mjini mshindi ni Esther Matiko mwenye kura 80 (97. 6%).
3. Tarime Vijijini mshindi ni John Heche ambaye amepata kura 268 (99.2%).

Heche alikuwa mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndiyo au Hapana, kwenye kura zilizopigwa, kura za Ndiyo ni 268 (99.2%), zilizoharibika ni 2 (0.74%) hapakuwa na kura ya Hapana
4. Mshindi Jimbo la Bunda Mjini ni Ester Bulaya  kura 126
5. Jimbo la Iramba mshindi ni Jesca Kishoa  kura 134 (98%).
Jesca alikuwa mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndiyo au Hapana, kwenye kura 136 zilizopigwa, kura za Ndiyo ni 134 (98%), zilizoharibika ni 2 na hakuna kura ya Hapana.
6. Jimbo la Isimani mshindi ni Patrick Ole Sosopi mwenye kura 115 (82.6%).
7. Mshindi jimbo la Mbeya Mjini ni Joseph Mbilinyi (Sugu) mwenye kura 294
– Sugu alikuwa ni mgombea pekee na alihitaji tu kura za Ndiyo au Hapana ambapo amepata Ndiyo 294 na Hapana 5.