MSIMAMIZI wa Uchaguzi katika Jimbo la Njombe Mjini amemtangaza Deodatus Philip Mwanyika wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo baada ya kupata kura halali 29,553.

Akitangaza matokeo hayo, msimamizi huyo amesema kuwa, wagombea wa Ubunge katika jimbo hilo walikuwa watatu kutoka vyama vya CCM, Chadema na DP.

Edward William (DP) – kura 162.

Emanuel Godfrey (Chadema)  – kura 5940.

Deodatus Philip Mwanyika (CCM) – kura  29,553

“Hivyo kwa mamlaka niliyopewa namtangaza, Deodatus Philip Mwanyika wa CCM kuwa ndiyo mbunge mteule wa Njombe Mjini,” amesema Msimamizi.