Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Saashisha Mafuwe, ameibuka mshindi katika Jimbo la Hai katika uchaguzi uliofanyika jana Jumatano, Oktoba 28, 2020.

 

Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, Yohana Elisha, ametangaza kuwa Mafuwe amepata kura 89,786 huku mpinzani wake Freeman Mbowe wa Chadema akipata kura 27,684 na wa tatu ni Mbaruku Mhina (ACT) mwenye kura 315.

 

Mbaruku Salehe Muhina (ACT Wazalendo) – kura 315

Saasisha Mafuwe (CCM) – kura 89,786

Freeman Mbowe (Chadema) – kura 7,684

Jumla ya kura zilizopigwa – 101785

 

Hivyo Mafuwe ametangazwa kuwa Mbunge Mteule wa Jimbo la Hai na kumburuza Mbowe aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo.