Jerry Silaa

 Jimbo la Ukonga, ameshinda Jerry Silaa, wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuwa ndiye mbunge wa jimbo hilo baada ya kupata kura 120,936 na kumshinda Asia Msangi wa Chadema aliyepata kura 21,634.
Jimbo la Temeke ameshinda Kilave Dorothy George kupitia CCM kuwa mshindi kwa kupata kura 192,756 akifuatiwa na Yahaya Omary (CHADEMA) kura 28,260.

Askofu Josephat Gwajima.

Jimbo la Kigamboni ameshinda Ubunge Jimbo wa CCM, Dr Faustin Ndungulile kwa kupata kura 34540, Lucy Mageleli (CHADEMA) amepata kura 11306, Mwanaisha Mndeme (ACT) Wazalendo 1952.

Jimbo la Kinondoni na Kawe, Aron Kagurumjuli amemtangaza mgombea ubunge wa CCM jimbo la Kinondoni Abass Tarimba ameshinda baada ya kupata kura 112,014.


Tarimba amewashinda wenzake 17 Kati ya hao Suzanna Lyimo wa Chadema amepata Kura 11260 na Said Kubenea wa ACT Wazalendo amepata Kura 5,948 na

 

Jimbo la Kawe ameshinda Askofu Josephat Gwajima wa CCM kuwa Mshindi wa Ubunge katika Jimbo hilo kwa kura 194,833 akifuatiwa na Halima Mdee (CHADEMA) mwenye kura 32,524.
Jimbo la Mbagala,  Abdallah Chaurembo ameshinda kura 283,000 akifuatiwa na Hadija Mwago (CHADEMA) mwenye kura 13,985 na Kondo Bungo (ACT) kura 3856.