Korea Kaskazini imefanya gwaride adimu la kijeshi wakati wa usiku wa Jumamosi, na kuhudhuriwa na kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un.

Gwaride hilo lilifanyika likiwa kumbukumbu ya miaka 75 ya Chama cha Wafanyakazi.

Waandishi wa habari wanasema kwamba makombora ya "makubwa" ya muda mrefu ambayo hayakuonekana yalioneshwa. Korea Kaskazini kawaida hutumia gwaride zake kuonesha makombora na silaha mpya.

Ni gwaride la kwanza nchini humo katika miaka miwili na inakuja wiki chache kabla ya uchaguzi wa urais wa Marekani.

Korea Kaskazini haikuwa imeonesha makombora ya masafa marefu katika gwaride zake tangu Rais Donald Trump na Bwana Kim walipofanya mkutano wao wa kwanza mnamo 2018.

Kulingana na jeshi la Korea Kusini, gwaride hilo lilifanyika kabla ya alfajiri Jumamosi. Sababu ya kufanyika mapema bado hazijulikani.

Korea Kusini ilisema ilifanya mkutano wa dharura wa Baraza lake la Usalama la Kitaifa Jumapili kujadili silaha zilizoonekana kwenye picha na yaliyomo kwenye hotuba hiyo na Bw Kim.

Ofisi ya rais wa Korea Kusini ilisema katika taarifa kwamba makubaliano baina ya Korea kuzuia mapigano ya silaha lazima yatekelezwe.

Hakuna vyombo vya habari vya kigeni au wageni waliruhusiwa kuhudhuria, kwa hivyo wachambuzi wanategemea picha zilizopigwa na vyombo vya habari vya ndani ambazo zinatolewa kutathmini gwaride hilo.

Kim Jong-un akipokea heshima Pyongyang (Oktoba 10)

Picha zilimuonesha Bw Kim akiwa amevaa suti ya kijivu ya mtindo wa Magharibi, akipokea maua kutoka kwa watoto.

Katika hotuba, alisema Korea Kaskazini itaendelea "kuimarisha" jeshi lake kwa "kujilinda".

Alisema pia anashukuru kwamba hakuna Wakorea wa Kaskazini walio na maambukizi Covid-19.

"Ninawatakia afya njema watu wote ulimwenguni ambao wanapambana na shida za virusi hivi viovu," alisema.

Licha ya kudai kuwa nchi hiyo haina mgonjwa wa korona, Bw Kim anaendelea kufanya mikutano ya kiwango cha juu kuhakikisha masharti mbalimbali yanabaki

Wachambuzi wamesema haiwezekani kwamba Korea Kaskazini haijapata maambukizi ya virusi vya corona.

Kombora

Wasiwasi

Uchambuzi wa Alistair Coleman, BBC Monitoring

Kwa kuona vifaa vya jeshi vikiwa katika viwanja vya Kim Il-sung kwenye runinga ya serikali, ni wazi kuwa hakuna gharama ambayo Korea Kaskazini haikuiingia kwa ajili vikosi vya jeshi vya Korea Kaskazini.

Wachambuzi waliotazama hafla hiyo iliyooneshwa mtandaoni watakuwa wameona wanajeshi wakiwa na silaha mpya za mashambulizi, pamoja na kile kinachoonekana kama mifumo mpya ya ulinzi wa anga na magari ya kivita.

Hatahivyo, ni kuonekana kwa makombora mapya ya masafa marefu ndiko kutakakosababisha wasiwasi zaidi.

Kwanza ilikuja kombora lililozinduliwa la nyambizi Pukguksong 4A, ikifuatiwa na kombora kubwa la Intercontinental Ballistic (ICBM) kwenye gari la kurushia na magari aina ya colossal 'axles' 11 mapya hatujui yamepewa majina gani

Ndege ya kijeshi ya Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imetumia mwaka uliopita au zaidi ikisema itaongeza uwezo wake wa nyukilia, na onyesho la ICBM katika gwaride la Jumamosi limetengenezwa kusisitiza ujumbe huu.

Hakukuwa na ishara ya mtu yeyote aliyevaa barakoa wakati wa gwaride. Hatahivyo kulikuwa na watu wachache sana waliohusika katika hafla hiyo kuliko kawaida, shirika la habari la AFP linaripoti.

Korea Kaskazini ilifunga mipaka yake na majirani mnamo Januari kuzuia maambukizi ya Covid-19 kuenea kutoka China na nchi jirani.

Mamlaka imeripotiwa kutoa maagizo ya "kuua kwa risasi" mpakani na kuzuia watu kuingia nchini humo.

Wanajeshi wakiwa mbele ya picha za of Kim Il-Sung na Kim Jong-il

Mwezi uliopita Bw Kim aliomba msamaha kwa shambulio baya dhidi ya raia wa Korea Kusini. Korea Kusini ilisema kwamba mtu huyo wa miaka 47 alipatikana na wanajeshi wakati akielea kwenye maji ya Kaskazini. Halafu alipigwa risasi na kufa na mwili wake ulichomwa moto, kulingana na Seoul.

Kwa wiki kadhaa, picha za setilaiti zimeonesha maelfu ya watu wakifanya mazoezi ya gwaride la Jumamosi.

Maafisa wa mambo ya nje huko Pyongyang waliambiwa waepuke kusafiri kupitia jiji hilo, kwenda karibu na eneo la tukio na kuchukua picha za hafla hiyo.