Donald n'umugore we Melania Trump

Trump na mke wake wamepatikana na virusi vya corona na sasa wako kwenye karantini.

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini.

Bwana Trump, 74, na hivyo basi yuko katika kundi lililo kwenye hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo, ameandika kwenye mtandoa wa Twitter: "Tutapita hili pamoja."

Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.

Tangazo hilo linawadia baada ya Bwana Trump na wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Aidha awali mke wa rais Melania Trump alituma ujumbe kuashiria kwamba wanaendelea vizuri.

''Kama ambavyo raia wengi wa Marekani wamefanya mwaka huu, Rais Trump na mimi tuko kwenye karantini nyumbani baada ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona. Tunaendelea vizuri na nimeahirisha shughuli zote zijazo. Tafadhali hakikisha uko salama na tutashinda changamoto hii pamoja.''

Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.

Bi. Hicks alisafiri na Bwana Trump kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni alipokabiliana na mpinzani wake Joe Biden Jumanne.

Baadhi ya familia ya Trump ilihudhuria mdahalo huo walionekana wakiwa bila barakoa.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Mapema Alhamisi, Bwana Trump alisema yeye na mke wake, 50, wanakwenda karantini baada ya Bi. Hicks kuthibitishwa kuwa na corona.

Ameandika kwenye mtandao wa Twitter: "Hope Hicks, ambaye amekuwa akifanyakazi kwa bidii sana bila hata kupumzika, amethibitishwa kuambukizwa ugonjwa wa Covid-19.

"Mke wangu na mimi tunasubiri matokeo yetu. Wakati huohuo, tutaanza mchakato wa kuwa kwenye karantini!"

Bado haijafahamika vile kuthibitishwa kwa Bwana Trump kutaathiri maandalizi ya mdahalo wa pili wa urais, ambao umepagwa kufanyika Oktoba 15 huko Miami, Florida.

Coronavirus
Banner

Bwana Trump mara nyingi huwa havai barakoa na amekuwa akipigwa picha akiwa hazingatii hatua ya kutokaribiana akiwa na wasaidizi wake au watu wengine wakati wa ziara zake rasmi.

Donald Trump
Maelezo ya picha,

Donald Trump akiwa kwenye mkutano wa kampeni

Kwa picha: Trump akifanya mkutano Minnesota

Siku moja tu kabla ya kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona, Rais Donald Trump alihudhuria mkutano wa siasa katika uwanja wa ndege wa Duluth, Minnesota.

Kama ambavyo imekuwa katika maeneo mengi ya umma, rais hakuwa akivaa barakoa.

Mikusanyiko haikuwa ikitekeleza hatua ya kutokaribiana na wengi wao, na wale waliohudhuria walionekana kutovaa barakoa.

Daktari wa Bwana Trump Sean Conley, alitoa taarifa ikisema rais na mke wake wote wanaendelea vizuri na wanapanga kusalia nyumbani ndani ya Ikulu wakati wa kipindi chao cha kuendelea kupona.

"Muwe na uhakika natarajia rais aendelee kutekeleza majukumu yake bila matatizo yoyote wakati anaendelea kupata afueni, na nitaendelea kuwafahamisha matukio yoyote ya siku za usoni," taarifa hiyo imesema.

Bwana Trump sio raisi wa kwanza duniani kukutwa na virusi vya corona. Mapema mwaka huu, Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Jair Bolsonaro wa Brazil walithibitishwa kuambukizwa.

Wote wawili wamepona ingawa Bwana Johnson alihitajika kupokea matibabu ya oksijeni mara kwa mara kusaidia mfumo wake wa upumuaji wakati akiwa hospitalini.

Uchambuzi na Anthony Zurcher, mwanahabari wa Amerika Kaskazini

Wiki moja baada ya Donald Trump kuwaambia raia wa Marekani kwamba wasiwe na wasiwasi kuhusu ugonjwa wa Covid-19 kwasababu "ni kana kwamba hauathiri yeyote" isipokuwa wazee na wenye matatizo ya moyo, rais mwenyewe amethibitishwa kupata maambukizi ya virusi vya corona.

Ni vigumu kuelezea ukubwa wa athari za tukio hili ikiwa zimesalia siku 32 tu kabla ya uchaguzi wa Marekani.

Rais atahitajika kuwa kwenye karantini kupata matibabu.

Mikutano ya kampeni sasa hivi imeisha. Mdahalo ujao wa urais uliopangwa kufanyika wiki mbili kutokea sasa, uko katika hali ya sintofahamu.

Ujumbe wa mara kwa mara kutoka kwa rais, kwamba taifa hilo linaelekea kukabiliana na virusi vya corona umepata doa baada ya yeye mwenyewe kuugua.

Ni siku mbili tu zilizopita, wakati wa mdahalo wa kwanza, Trump alimdunisha mpinzani wake Joe Biden kwa kuvaa barakoa mara kwa mara na kwa kutokuwa na mikutano ya kampeni inayoendana na hadhi yake.

Sasa hivi, Ikulu ya Marekani na timu ya kampeni zitahitajika kujibu swali la kwanini rais alikuwa na mwenendo wa aina hiyo kwa misingi ya kujikinga yeye mwenyewe - na ni wangapi wengine katika Ikulu ya Marekani na wengine wa ngazi ya juu serikalini huenda wameathirika.

Wakati wa msukosuko wa kitaifa, raia wa Marekani wanaonekana kupendelea upande wa rais. Ingawa hilo, huenda isitoshe kuondoa uwezekano wa kujibu maswali yatakayofuata.

Trump amesema nini kuhusu virusi vya corona?

Marekani ina idadi kubwa ya vifo vilivyotokana na virusi vya corona. Lakini rais Trump anasisitiza kwamba alikabiliana vilivyo na janga hilo tena kwa njia stahiki.

Yafuatayo ni baadhi ya semi zake kuhusu virusi vya corona.

Januari 22 - Maambukizi ya kwanza ya virusi vya corona kuthibitishwa Marekani "Tumeudhibiti"

"Tumeudhibiti kabisa. Ni mtu mmoja tu anayetokea China. Tumeudhibiti. Hali itakuwa sawa."

Machi 9 - Alilinganisha virusi vya corona na mafua

"Kwahiyo mwaka jana raia 37,000 wa Marekani walifariki dunia kutoka na homa. Wastani wake ni kati ya 27,000 na 70,000 kwa mwaka. Hakuna ambacho kimesitishwa, maisha na uchumi yanaendelea... Fikiria kuhusu hilo!"

Machi 31- "Hii sio homa"

"Sio homa. Ni ukatili. Unapompeleka rafiki yako hospitalini... inakuwa ndio kwaheri, mkakamavu, mzee kiasi, mzito kidogo kuliko alivyotaka kuwa. Na ukipiga simu siku inayofuata kuuliza, 'anaendeleaje?' Amepoteza fahamu? Hii sio homa."

Aprili 3 - "Kuchagua kutovaa barakoa"

"Kuvaa barakoa, litakuwa jambo la kuchagua mwenyewe. Unaweza kufanya hivyo lakini sio lazima. Mimi sitavaa, nachagua kutovaa barakoa, lakini wengine huenda wakataka kuvaa na hivyo pia ni sawa"

Julai 21 - "Vaa barakoa"

"Tunamtaka kila mmoja ambaye atashindwa kutekeleza hatua ya kutokaribiana, kuvaa barakoa, vaa barako."

Septemba 10 - Tunakaribia kukabiliana " na janga

"Tunakaribia kukabiliana na janga, na mengine mengi mazuri yanaendelea kutokea kuhusu chanjo na tiba"