MAHAKAMA ya Haki ya Afrika Mashaki inatarajiwa kuamua kesi inayopinga uhalali wa Yoweri Museveni kugombea tena urais wa Uganda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021.

 

Mahakama ya juu zaidi ya Uganda iliidhinisha marekebisho ya katiba ili kuondoa ukomo wa miaka kwa wagombea wa urais. Marekebisho ya katiba ya mwaka 2017 iliondoa kifungu cha sheria kinachowataka wagombea uraisi kuwa na umri wa chini ya miaka 75.

 

Hatua hiyo ilimruhusu rais Yoweri Museveni, ambaye ana umri wa miaka 75, kugombea mhula wa sita katika uchaguzi wa Januari mwaka 2021. Amekuwa madarakani tangu mwaka 1986.