MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva na mchumba wa sexy lady kunako Bongo Fleva ni, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’, William Lymo ‘Billnass’, amejibu swali tata lililotokana na wimbo wao wa Do Me,CHANZO  kinakupa habari zaidi.

 

Wimbo huo wa Do Me ni wa Nandy akiwa amemshirikisha Billnass au Bilinenga ambapo mstari ulioibua swali hilo ni ule unaosema; “Nafikiri kuhusu suti, sifikirii kutumia kinga hata waseme una virusi.

“Viuno vingi kama Christian Bella

Peace ya msela

African Princess Nandela (jina la utotoni la Nandy).”

 

MASWALI KIBAO

Mstari huo umeibua maswali kama yote kwenye mitandao ya kijamii ambapo wadau mbalimbali walihoji kulikoni? Kuna ukweli wowote juu ya alichokiimba Billnass?

 

“Nandy na Billnass walitangaza kuachana na sasa tumeona wimbo halafu kwa nini Billnass aseme hata kama ana virusi hafikirii kutumia kinga?’’ Alihoji shabiki mmoja.

Wengine walikwenda mbali zaidi kwa kuhoji, kwani Nandy ameambiwa ana virusi? Kwa nini Billnass aseme; “Sifikirii kutumia kinga hata waseme una virusi!”

 

BILLNASS AJIBU SWALI HILO…

Baada ya mambo kuwa mengi mitandaoni huku kila mmoja akisema lake hasa juu ya uchumba ‘sugu’ wa Billnass na Nandy, Gazeti la IJUMAA lilifanya jitihada za kumtafuta Billnass na kufanya naye mahojiano maalum ambapo alijibu maswali kuhusu ishu hiyo;

IJUMAA: Mambo vipi Billnass?

 

BILLNASS: Poa tu niambie…

IJUMAA: Hongera sana, wewe na Nandy kwa kuachia ngoma kali ambayo inakimbiza mitandaoni kwa sasa…

BILLNASS: Namshukuru Mungu na mashabiki pia kwani imekuwa na mapokeo makubwa maana zimetoka nyimbo nyingi na nzuri zaidi, lakini imepenya.

 

IJUMAA: Katika utunzi wa mashairi wewe ndiye ulihusika?

BILLNASS: Hapana, si yote, katika mistari ya Nandy ameandika Jay Melody (msanii wa Bongo Fleva), ila mistari yangu nimeandika mwenyewe.

IJUMAA: Kuna mstari umeimba ambao unasema; “Situmii kinga hata waseme una virusi.” Je, ni kwa nini umeimba hivyo?

 

BILLNASS: Ni lugha ya mfananisho kwenye muziki, ni sawa na mtu aseme kwamba mimi simba au chui anaweza kubadilika hapohapo? Hakuna, ni mfanano wa lugha tu. Kwangu mimi nilikuwa ninazungumzia ni jinsi gani nimejitolea (risk) nitakayoichukua, kwa sababu HIV ni gonjwa baya na hatari na unapaswa kuliepuka.

Hata kama kuna uvumi au shaka kiasi gani, mimi niko tayari kumuoa.

IJUMAA: Je, kuna uvumi ulisikia kuwa Nandy ana virusi ndiyo ukaamua kuimba hivyo?

 

BILLNASS: Nimekwambia ni lugha ya mfananisho na mimi nimeamua kubadilisha kwa lugha nyingine sawa na mtu aseme; “Nipo tayari kufa kwa ajili yako!” Maana yake ni maneno ambayo yameshatumika sana na haiwezekani kila msanii aimbe hivyo ndiyo maana nimebadilisha.

IJUMAA: Baada ya hii kuna kolabo yenu nyingine inakuja?

BILLNASS: Kazi nyingi zinakuja na zitakuwa nzuri zaidi, mashabiki wetu wategemee vikubwa na muda ukifika tutatoa tu.

 

TUJIKUMBUSHE

Hivi karibuni, Nandy na Billnass walizua tafrani mitandaoni baada ya kusambaa kwa tetesi kuwa wameachana kiasi cha Nandy kuvua pete ya uchumba aliyovalishwa na Billnass.

Wimbo wa Do Me waliuachiwa rasmi Oktoba 22, mwaka huu na kukimbiza kwenye Mtandao wa YouTube kwa kushika trending namba moja ukiwa umetazamwa mara zaidi ya milioni moja hadi sasa.

 

MAUDHUI YA DO ME

Wimbo wa Do Me ambao umepita kwenye mikono ya Producer Kimambo, ina maudhui ya kimapenzi kati ya watu wawili wapendanao ambao wanajibizana.

 

UBUNIFU

Kuanzia video ya wimbo huo ambayo imepikwa na Director Elvis, imekuwa na ubunifu wa aina yake kwani wapendanao hao wamejua kwenda sambamba na maudhui ya wimbo huo.

Lokesheni yake iko poa kutokana na uchaguzi wa mavazi na rangi zilizotumika kwenye video hiyo.

Billnass na Nandy ni vijana wapambanaji walioamua kutumia vipaji vyao kusaka mkate wao wa kila siku.