WAZIRI wa mambo ya nje wa zamani wa Marekani Colin Powell amefariki dunia kwa  ugonjwa wa Covid-19, Powell ambaye alikuwa Mmarekani wa kwanza mwenye asili ya Afrika kushika wadhifa wa waziri wa mambo ya ndani ya Marekani amefariki dunia akiwa na miaka 84.

Powell alihudumu chini ya Rais George Bush, kati ya mwaka 2001-2005 ,taarifa ilisema kwamba alikuwa amepata chanjo dhidi ya ugonjwa huo kabla kifo chake Powell alikuwa mshauri wa kijeshi kwa viongozi wengi wa kisiasa.

 

Alishiriki kwenye vita  nchini Vietnam, uzoefu ambao baadaye ulimsaidia kuandaa mipango yake ya kijeshi na kisiasa.

 

Alikuja kuwa mshauri wa kijeshi aliyetegemewa na wanasiasa kadhaa nchini Marekani pia alikuwa na mchango mkubwa wakati wa uvamizi wa mwaka 2003 nchini Iraq.

 

Colin Luther Powell alizaliwa Harlem, New York tarehe 5 Aprili mwaka 1937 akitoka kwenye familia ya wahamiaji wa Jamaica.