Takriban watu sita wameuawa na wengine 32 kujeruhiwa na risasi katika mji mkuu wa Beirut nchini Lebanon.
Yote haya yalianza wakati wa maandamano yaliofanywa na makundi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia , Hezbollah na Amal dhidi ya jaji mmoja aliyekuwa akichunguza mlipuko mkubwa mwaka jana katika mji huo wa bandari.
Walisema kwamba wanajeshi wa kuvizia wa dini ya Kikristo kutoka kwa jeshi la Lebanon LF walifyatua risasi katika kundi moja la watu kwa lengo la kuishinikiza Lebanon kuingia katika ghasia - madai yanayopingwa na jeshi hilo.
Hali ya wasiwasi inazunguka uchunguzi uliosababisha mlipuko huo uliowaua watu 219. Wapiganaji wa Hezbollah na washiriki wake wanadai kwamba jaji huyo anapendelea, lakini familia za waathiriwa wanaunga mkono kazi yake.
Hakuna hata mtu mmoja ambaye amepatikana na hatia ya mlipuko huo wa Agosti 2020, ambapo maeneo mengi ya mji huo yaliharibiwa vibaya.
Akijibu mashambulizi ya siku ya Alhamisi , ambayo yameonekana kuwa mabaya zaidi katika miaka ya hivi karibuni, waziri mkuu Najib Mikati alitangaza siku ya kuomboleza siku ya Ijumaa.
Wakati huohuo, Rais Michel Aoun alisema: Hatutaruhusu mtu yeyote kuliteka nyara taifa hili kwa maslahi yao ya kibinafsi.
Kile kilichoanza kama maandamano nje ya kasri la haki - jengo kuu la mahakama - ambapo mamia ya wakaazi walikuwa wakikosoa uchunguzi huo -kilishinikizwa kisiasa na kuwataka raia kutaka jaji huyo Tarek Bitar kuondolewa, kulingana na mwandishi wa BBC Anna Foster mjini Beirut.
Ufyatulianaji wa risasi ulizuka katika barabara za mji huo wakati kundi hilo la watu lilipokuwa likivuka mzunguko wa barabara katika eneo la katikati mwa mji la Tayouneh- Badaro.
Wakaazi walilazimika kutoroka makazi yao huku wanafunzi wakikimbilia maeneo ya kujificha chini ya madawati yao huku watu waliokuwa wamejihami na bunduki pamoja na magurunedi , wanaoaminika kuwa wanachama wa dhehebu la Shia pamoja na Wakristo walipofyatuliana risasi barabarani.
Ghasia ziliendelea kwa saa kadhaa kabla ya utulivu kurudi.
Katika shule moja, walimu waliwaagiza watoto kulala wakiangalia chini ardhini huku mikono yao ikiwa kichwani , shahidi mmoja alikimbia chombo cha habari cha Reuters.
Mwisho wa Twitter ujumbe, 1
Vyanzo vya Hopsitali na vile vya kijeshi vilisema kwamba baadhi ya wale waliouawa walipigwa risasi kichwani.
Walikuwa pamoja na mwanamke mmoja ambaye alipigwa risasi akiwa ndani ya nyumba yake.
Makundi hayo mawili ya kishia yalisema waandamanaji walikuwa "wahanga wa shambulio lililofanywa na vikosi vya chama cha Lebanon vilivyopelekwa katika barabara za mji huo pamoja na walengaji shabaha waliokuwa juu ya mijengo ambao walikuwa wakifanya mauaji ya kukusudia ".
Kiongozi wa vikosi vya Lebanon Samir Geagea amelaani ghasia hizo na kutoa wito wa utulivu.
"Sababu kuu inayochangia hali hii ni uwepo wa silaha zisizodhibitiwa na zilizoenea ambazo zinatishia maisha ya raia wakati wowote na mahali," aliandika kwenye Twitter tweeted.
Bw. Mikati ametoa wito kwa watu wote kuwa "watulivu na kujiepusha na visa vyovyote vya uasi".
Jeshi limesema lilikuwa limepeleka vokosi vyake kuwatafuta washambuliaji , na kuonya kuwa"watampiga risasi mtu yeyote atakayepatikana na bunduki barabrani".
Mapema siku ya Alhamisi, mahakama ilitupilia mbali malalamiko ya kisheria yaliyowasilishwa na mawaziri wawili wa zamani wa serikali na wabunge wa Amal - Ali Hassan Khalil na Ghazi Zaiter - ambao Jaji Bitar alitaka wahojiwe juu ya tuhuma za uzembe kuhusiana na mlipuko wa bandari.
Wanaume hao ambao walikana kufanya makosasa yoyote , walimshtumu jaji huyo kwa upendeleo,
Familia za waathiriwa zililaani malalamishi hayo, ambayo yalisababisha uchunguzi kusitishwakwa mara ya pili ndani ya wiki tatu.
Wameshutumu uongozi wa kisiasa wa nchi hiyo kwa kujaribu kujikinga dhidi ya uchunguzi.
Mlipuko wa bandarini ulitokea baada ya moto kusababisha tani 2,750 za kemikali ya ammonium nitrate, ambayo hutumiwa kutengeza mbolea, ambayo ilikuwa umehifadhiwa visivyo katika bohari yam bandari hiyo kwa karibu miaka sita kulipuka.
Maafisa wa ngazi ya juu walikuwa na ufahamu juu ya uwepo wa kemikali hiyo na hatari iliyowakodolea macho isipohifadhiwa vyema, kuondolewa au kuharibiwa
0 Comments