RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwahutubia Waumini wa Dini ya Kiislam katika hafla ya Ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa inayofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja jana 22-10-2021.(Picha na Ikulu) 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiitikia dua maalum iliyosomwa na Amiri Lulu kutoka Gongolamboto Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na (kulia kwa Rais) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Saleh Omar Kabi na Amiri Mkuu Ali Khamis Mwalim na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman.(Picha na Ikulu)

WAUMINI wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiitikia Dua ikisomwa na Amiri Lulu kutoka Dar es Salaam, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa iliofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar, kabla ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa iliofanyika leo.(Picha na Ikulu) 

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman, akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa iliofanyika katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikulu) 

Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi, kufungua Ijitimai ya Kimatifa, inayofanyika katika Masjid FDiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.(Picha na Ikuu)


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj. Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Dini alipowasili katika Masjid Fiysabilillahi Tabligh Markaz Zanzibar Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Ijitimai ya Kimataifa 2021, inayofanyika leo 22-10-2021.(Picha na Ikulu)