Rais Samia ametangaza awamu ya tatu ya chanjo ya Covid
Tanzania inatarajia kupokea awamu ya tatu ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 baada ya kupokea awamu mbili za awali ili kukabiliana na ugonjwa huo unaoua.
Awamu hiyo ya chanjo inakuja baada ya nchi hiyo kupokea chanjo ainia ya Johnson and Johnson zaidi ya dozi milioni moja kutoka Marekani chini ya mpango wa Covax, pia chanjo nyingine zaidi ya milioni moja aina ya Sinopham kutoka China.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza awamu hiyo ya chanjo alipohutubia mkutano wa hadhara mjini Arusha Kaskazini mwa nchi hiyo na kusema chanjo za awamu ya kwanza zimetumika kwa asilimia 88. Hata hivyo, hakutaja aina ya chanjo inayotarajiwa kupokewa.
Chini ya Rais Samia aliyechukua madaraka Machi 19 mwaka huu, Serikali imeweka msisitizo wa chanjo kama moja ya njia muhimu za kukabilianana UVIKO-19. Mtangulizi wa Samia, John Magufuli aliyefariki Machi 17 alikuwa na msimamo tofauti juu ya chanjo huku akielekeza wataalamu wake kujiridhisha, akidai baadhi ya chanjo si salama kwa watanzania.
Hata hivyo hali ilibadilika Julai 28 mwaka huu ambapo Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan binafsi alipata chanjo dhidi ya Corona .
Samia aliwaongoza maafisa wengine wa serikali wakiwemo Waziri mkuu Kassim Majaaliwa kupokea chanjo hiyo .
Katika uzinduzi wa hafla ya chanjo chini humo rais Samia alisema serikali yake itahakikisha kwamba kila mtanzania nayetaka kuchanjwa anapata chanjo hiyo .
'Mimi ni mama ya watoto wanne,mimi ni bibi wa wajukuu kadhaa na pia mimi ni mke ..siwezi kujiweka katika hatari … Nimekubali kwa hiyari yangu na najua ndani ya mwili wangu nina chanjo kadhaa na nimeishi nazo kwa miaka karibu 61' alisema rais Samia kabla ya kuchanjwa.
Katika hotba yake wakati wa uzinduzi huo rais Samia aliwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo akisema kuna walioathiriwa na kuwapoteza jamaa zao ambao wangefurahia kuipata chanjo hiyo mapema.
' Wakati gonjwa hili linapokuguza ndipo utajua hatari yake…nenda Moshi,nenda Kagera ,nenda Arusha..wana maneno ya kukuambia' alisema Rais Samia.
0 Comments