Lulu Diva anasema mama yake alikuwa anampa sapoti kubwa kwenye mambo anayoyafanya pia alikuwa anatamani kufanya vitu vingi lakini hali ya afya na umri ulikuwa haumruhusu

Akimzungumzia mama yake enzi za uhai wake Lulu Diva anasema ni mama ambaye alikuwa anamsihi asikate tamaa, afanye bidii na kuendelea kufanya kazi

Pia amesema mama yake alikuwa anamwambia asifananishe kifo na usingizi kwa sababu yeye ni mtoto wa kimaskini hivyo apambane asijifananishe na matajiri.


Taarifa za kifo cha mama Lulu Diva zimetoka siku ya jana na msiba upo Kunduchi Dar es Salaam karibu na kota za jeshi.