Jopo la wanasayansi kwa ushirikiano na Shirika la anga za mbali la Ulaya (ESA) kwa ushirikiano na Shirika la anga za mbali la Urusi (Roscosmos) wametangaza uvumbuzi wa kiwango kipya kikubwa cha maji katika sayari ya Mars.

Maji hayo yamemepatikana kwenye sakafu ya korongo la Valles Marineris , wenye korongo kubwa na lenye kimo kirefu zaidi katika mfumo wa jua.

Chanzo hicho kiligunduliwa na setilaiti unaofahamika kama Trace Gas Orbiter (TGO), ambao umekuwa ukifanya uvumbuzi kwenye sayari ya Mars tangu mwaka 2016 kwa kutumia kipimo cha Fine Resolution Epitermal Neutron Detector (FREND). ) ambacho kitaruhusu kupimwa kwa hydrogen kwa hadi mita 1 chini ya sakafu ya Mars.

ภาพจำลองดาวเทียม Trace Gas Orbiter ที่โคจรสำรวจรอบดาวอังคาร

CHANZO CHA PICHA,ESA / EXOMARS / TGO

Maelezo ya picha,

Picha ya setilaiti ya Trace Gas Orbiter ikizunguka sayari ya Mars.

Dkt. Igor Mitrofanov, kiongozi wa jopo la wanasayansi wananaotumia kifaa cha FREND, alisema: "Tuliweza kupenya hadi mita moja chii ya sakafu ya vumbi jekundu na kupata kiwango kikubwa sana cha haidrojeni katika eneo la korongo la Valles Marineris."

"Haidrojeni hii ni kiungo cha chembembe za maji. Na inaonekana kuwa hadi 40% ya eneo la sakafu yenye maji ya madini."

Eneo ambako maji mapya yaligundulika, linaloitwa Candor Chasma, liko katikati ya korongo lililo wazi. Katikati ya korongo la Valles Marineris, eneo hili lina ukubwa sawa na nchi ya Uholanzi.

Picha: Kiasi kikubwa cha maji kimepatikana chini ya sakafu ya Candor Chasma, eneo la wazi la korongo la Valles Marineris.

Unaweza pia kusoma:

พบแหล่งน้ำขนาดใหญ่ใต้พื้นผิวของ Candor Chasma ซึ่งเป็นที่ลุ่มในหุบผาส่วนที่เปิดกว้างของ Valles Marineris

CHANZO CHA PICHA,ESA / DLR / FU BERLIN

Maelezo ya picha,

Kiwango kikubwa cha maji kimepatikana chini ya ardhi ya leno la Candor Chasma, lililopo kwenye korongo la Valles Marineris

Dkt Alexei Malakov, mtafiti mwingine wa ngazi ya juu katika jopo hilo, aliongeza: : "Ni kiasi gani cha maji kitakuwa pale? Hii inategemea kiwango cha neutroni kilichoachiwa wakati chembe za joto la juu lililosababishwa na miale lilipogongana na sakafu. Ardhi kavu hutoa neutron zaidi ya ardhi yenye unyevu."

"Maji tunayoyapata hapa yana uwezekano mkubwa wa kuwa sawa na barafu iliyo chini ya sakafu ya dunia, lakini kunaweza kuwa na sababu nyingine zinazoyaruhusu kuwa chini ya ardhi kavu ya chini ya Ikweta, ambayo ina joto la juu kuliko maeneo ya nyota ." Zaidi ya hayo, kimo kirefu cha maji chini ya sakafu ya nyota pia kinaleta matumaini kwamba maji hayo yanaweza kutumiwa kwa kunywa , iwapo wataalamu wa anga za mbali watatumwa kwa uvumbuzi wa muda mrefu ," said Dkt. Malakov.

Korongo la Valles Marineris lililopo katika sayari ya Mars au "Grand Canyon" lina urefu kilomita 4,000 , likiwa kwenye ikweta . Likilinganishwa na Korongo kubwa zaidi katika dunia, Korongo hilo lilikuwa na karibu urefu mara kumi, upana mara 20, na kimo kirefu ara tano zaidi.

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video,

Shimo Jeusi lililogunduliwa angani