Jeshi la Ethiopia limedhibiti tena mji wa kihistoria wa Lalibela kutoka kwa waasi wa Tigray.

Hatua hiyo imekuja huku kukiwa na tangazo la kundi la (TPLF) kwamba linajiondoa katika maeneo yote katika maeneo ya Amhara na Afar.

TPLF limesema lilichukua uamuzi huo ili kusafisha njia ya suluhu la amani la mgogoro wake na serikali.

Mzozo huo umesababisha mzozo mkubwa wa kibinadamu, huku juhudi za upatanishi za kimataifa hadi sasa zikishindwa.

Haijulikani ni lini wanajeshi waliuchukua tena mji wa Lalibela, lakini Naibu Waziri Mkuu Demeke Mekonnen Hassen alitembelea mji huo, huko Amhara, Jumapili.

Lalibela, maarufu kwa makanisa yake ya mwamba ambayo yalianza karne ya 12 na 13, iliteuliwa kuwa kituo cha urithi wa ulimwengu cha UNESCO mnamo 1978.

Mji huo umebadilishwa mikono mara kadhaa tkati ya serikali na waasi tangu Agosti.

Siku ya Jumamosi, serikali ilisema wanajeshi wake wamechukua tena miji mingine kadhaa, pamoja na Weldiya.

TPLF imekuwa ikiwaondoa wapiganaji wake kutoka maeneo ya vita na kuwarejesha kwenye ngome yake ya Tigray baada ya kulazimishwa kuachana na mpango wake wa kusonga mbele hadi mji mkuu wa Addis Ababa.

Ilisema uondoaji huo ulikuwa sehemu ya "marekebisho muhimu" ambayo ilikuwa ikifanya, ingawa haikuthibitisha kuwa imejiondoa kutoka kwa Lalibela na Weldiya.

Maelezo ya video,

Makanisa yanayoutambua mji wa Lalibela

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amekuwa mstari wa mbele kuongoza mapambano dhidi ya TPLF. Kundi hilo pia lilikuwa limekumbwa na mashambulizi ya anga.

Maelfu ya watu wameuawa, mamilioni wameachwa bila makao na karibu milioni 10 wanahitaji msaada wa chakula.

Mapigano yalizuka zaidi ya mwaka mmoja uliopita kati ya wanajeshi wa serikali na TPLF kufuatia mzozo mkubwa kuhusu mageuzi ya kisiasa yaliyoletwa na Bw Abiy alipoingia madarakani mwaka wa 2018.

TPLF ilikuwa imetawala serikali kuu kwa zaidi ya miaka 25, na sasa inadhibiti sehemu kubwa ya Tigray.

Map