Mary Stephano ni mlemavu wa miguu ambaye shughuli yake kubwa ni ombaomba, kazi anayoifanya katikati ya jiji la Mwanza.

Mary amesema katika kazi hiyo ambayo anaendelea kuifanya amefanikiwa kujenga nyumba mbili (na zenye wapangaji zaidi ya 20), kununua viwanja vitatu na kufungua Bar, kusomesha mtoto wake katika chuo cha uhazili Tabora.

Mary ni mama wa watoto wanne (wakike mmoja) ambao wote aliwapata na baba tofauti, mme wake anayeishi nae kwa sasa ana watoto 12 ambao na yeye aliwapata kwa mama tofauti kabla ya kukutana na mama huyo.