MAHAKAMA ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro imemuhukumu kwenda jela miaka 30, Elitumain John Elitumain miaka 31 mkazi wa kitongoji cha Majengo Kata ya Hedaru Wilayani hapa Kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 12.
Akitoa hukumu hiyo leo Desemba 24, hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Mussa Hamza amesema mtuhumiwa alifikishwa mahakamani hapo akiwa na kesi ya kumbaka binti huyo ambaye alikuwa mfanyakazi wa ndani nyumbani kwake.
Hakimu Hamza amesema kulingana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na Jamuhuri wakiongozwa na waendesha mashtaka wa Serikali, Frank Masese na Samweli Flavian wamethibisha pasipo shaka kuwa kosa hilo lilitendeka Oktoba 27, 2021 huko nyumbani kwa mshtakiwa.
Mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa hilo kwa mujibu wa kifungu cha sheria 130 (2) (e) na 131(1) vyote vikiwa ni kanuni ya adhabu mapitio ya mwaka 2019 shauri la jinai 132/2021.
0 Comments