WATU watatu waliokuwa wakisafiri kutoka Kata ya Nzera kuelekea Geita Mjini wakitumia gari la abiria (aina ya Toyota Hiace) wamefariki dunia papo hapo na wengine nane kujeruhiwa baada ya gari lao kugongana na Lori katika eneo la Pori la Mgodi wa GGM Wilayani Geita Mkoani Geita.
Akithibitisha vifo hivyo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Geita ambayo ndio imepokea mii ya marehemu hao na kuihifadhi, Dk. Paschal Thumba amesema walipokea miili hiyo ya watu watatu huku wengine wakipewa rufaa ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza.
Taarifa zaidi tutaendelea kukujuza………
0 Comments